Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Waumini watano wa dini ya kikristo akiwemo Padri mmoja watekwa nyara kaskazini mwa Mali.

Watu watano ambao ni waumini wa dini ya kikristo akiwemo Padri Leon Dougnon wametekwa nyara kaskazini mwa Mali. Walikuwa njiani katika jimbo la Mopti wakati wakielekea kwenye mazishi ya kasisi wa zamani wa Parokya, katika Jimbo la Segou, hadi sasa hawajapatikana.

Mali : rais Ba N'Daw et Moctar Ouane wakati wa mkutano wa usalama jijini Bamako Juni 2021
Mali : rais Ba N'Daw et Moctar Ouane wakati wa mkutano wa usalama jijini Bamako Juni 2021 © AP
Matangazo ya kibiashara

Eneo hilo limekuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji wa kundi la kijihadi la Katiba Macina lenye mafungamano na Al Qaeda.

Rafiki yake alipojaribu kuwasiliana na Padri Léon kwenye simu yake asubuhi mapema, sio yeye aliyejibu simu hiyo.

Padri Kizito Togo, kasisi wa parokia ya kanisa kuu la Mopti, anaeleza hapa namna alivyopata tarifa za tukio.

Kasisi huyo anasema padre pamoja na watu walioondoka pamoja waliunda ujumbe wa watu watano na kuondoka kuenda kwenda kwenye mazishi kuanzia jumatatu na hawakufika Mopti, hivyo wakaanza kuingiwa na wasiwasi, hali ambayo iliwapelekea kupiga simu.

Togo anaongeza kuwa watu hao walionekana kati ya Segue na Banyagara, padre wa segue kuenda Mopti inabidi apitie hapo Banyagara. Mtu aliyepokea alipoitikia kwa neno : Asalaam aleikum wakati si kawaida ya padre huyo, ndipo ilibainika kuwa walitekwa

Tukio hilo la utekaji lilithibitishwa na viongozi wa eneo hilo ambapo mpaka sasa hakuna kundi lolote lilijitokeza na kuthibitisha kuhusika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.