Pata taarifa kuu

Mali: Wanajihadi washambulia Kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa wa operesheni Barkhane.

Maafisa wa usalama nchini Mali wamethibitisha kuwa waanajeshi kadhaa wa ufaransa wamejeruhiwa katika shambulio la bomu eneo la Gossi katikati mwa Mali siku ya Jumatatu baada ya gari lao kukanyaga bomu wakati wakipiga doria katika operesheni Barkhane.

Wanajeshi wa ufaransa katika operesheni Barkhane wakipiga doria nchini Mali.
Wanajeshi wa ufaransa katika operesheni Barkhane wakipiga doria nchini Mali. © AFP/Pascal Guyot
Matangazo ya kibiashara

Mashuhuda wanasema gari lililokuwa limewabeba askari wa Ufaransa ikiwa ni sehemu ya kikosi kinachoendeleza operesheni zinazolenga kuwatimua wanajihadi katika êneo la Sahel liligongana na gari lililopakiwa mabomu.

Tukio hilo lilitokea eneo lisilo mbali na zahanati inayofahamika kama Anne-Marie Salomon, iliyopewa jina la mtawa wa kifaransa ambaye ameanzisha kituo cha afya kuwatibu wakaazi wa eneo hilo.

Afisa wa jeshi la Mali ambaye ameithibitisha taarifa hiyo kwa masharti ya kutotajwa jina, amefahamisha kuwa wanajeshi watatu wa Ufaransa waliojeruhiwa, walihamishwa na helikopta kwenda kituo cha Barkhane huko Gao.

Haya yanajiri wakati viongozi kutoka jumuiya ya nchi za kiuchumi za Afrika Magharibi ECOWAS ambao walikutana jijini Accra nchini Ghana mwishoni mwa juma lililopita, kujadili hali ya kisiasa nchini Mali, wamesema wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya uongozi wa mpito nchini kabla ya kuondoa hatua ya kuisimamisha uanachama wa Jumuiya hiyo.

Rais wa mpito kanali Assimi Goita ametangaza serikali ya kiraia na kuahidi kuheshimu mipango ya kuandaa uchaguzi Mkuu nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.