Pata taarifa kuu

Waziri Mkuu mpya nchini Mali ahimiza serikali yake kutimiza malengo

Siku ya Jumapili huko Bamako, mji mkuu wa Mali, waziri Mkuu  Choguel Kokalla Maïga, alikusanya serikali yake kwa mara ya kwanza ili kuipatia ramani na kuitaka kutekeleza majukumu yake lakipia kuyatimiza kabla ya uchaguzi wa Februari 2022 muda uliopangwa kurejesha utawala wa kiraia.

Luteni-Kanali Abdoulaye Maiga, Waziri wa Utawala wa Wilaya na Ugawaji Madaraka, na Kanali Meja Ismael Wagué, Waziri wa maridhiano ya Kitaifa, wakati wa mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri la serikali mpya ya Mali mnamo Juni 13, 2021.
Luteni-Kanali Abdoulaye Maiga, Waziri wa Utawala wa Wilaya na Ugawaji Madaraka, na Kanali Meja Ismael Wagué, Waziri wa maridhiano ya Kitaifa, wakati wa mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri la serikali mpya ya Mali mnamo Juni 13, 2021. © Kaourou Magassa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Mali Choguel Kokalla Maïga amesema, miongoni mwa majukumu hayo ni pamoja na kuundwa kwa chombo kimoja huru cha usimamizi wa uchaguzi, kinachodaiwa na jamii ya kisiasa na asasi za kiraia nchini humo, kesi halisi za kisheria kufuatia mauaji na dhuluma dhidi ya wahanga wa siku ya Julai 2020 pia litazingatiwa.

Choguel Kokalla Maïga ambae aliteuliwa kwa wadhifa huo na Kanali Assimi Goita tangu mapinduzi, ameseka wazi vipaumbele vyake.

ikiwa ni pamoja na kuboreshwa kwa usalama, mageuzi ya kisiasa na taasisi na kuandaa uchaguzi wa kuaminika.

Dhamira hii mpya ya serikali inakuja wakati Mali imekuwa ikipambana kwa miaka mingi dhidi ya makundi ya kijihadi.

Ufaransa, mshirika wake katika mapigano haya, ilitangaza Alhamisi mwisho wa siku zijazo wa Operesheni Barkhane huko Sahel kwa kuunga mkono muungano wa kimataifa.

Waziri Mkuu na rais wa mpito bado hawajaelezea hadharani juu ya uamuzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.