Niger yatangaza nia yake ya kushirikiana na Chad dhidi ya waasi wa FACT
Kulingana na jeshi la Chad, Idriss Déby inawezekana kuwa kifo chake kilitokana na majeraha aliyoyapata katika makabiliano kati ya vikosi vya jeshi la serikali na waasi wa FACT alipokuwa akiongoza mapigano Jumatatu Aprili 19.
Imechapishwa:
Baraza la Kijeshi la Mpito, ambalo linakataa makubaliano yoyote au mazungumzo yoyote na kundi la waasi la FACT, linahakikisha kwamba waasi hao walikimbilia katika nchi jirani ya Niger na kuomba ushirikiano wa Niamey ili kuwaangamiza.
Kutoka chanzo rasmi nchini Niger, sasa inasemekana kuwa nchi hiyo inashirikiana kikamilifu na Chad. Kulingana na chanzo hicho, vikosi vya jeshi vya nchi hizo mbili vinawasiliana vya kutosha. Baadhi ya watu wamekamatwa katika eneo la Darkou, bila hata hivyo kutaja idadi yao kwa wakati huu.
Siku ya Jumapili Aprili 25, msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito (CMT) alithibitisha kwamba waasi wa Front for Alternation and Concord in Chad (FACT) walisambaratishwa na vikosi vya jeshi vya Chad, na kwamba walikimbilia nchini Niger. Jenerali Azem Bermandoa Agouna alisema wako tayari kuwasaka, na aliomba ushirikiano wa Niger, na washirika wa G5 Sahel.