Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI-DIPLOMASIA-SIASA-ZIARA

Kaimu Waziri Mkuu wa Ubelgiji atembelea DRC

Kaimu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Sophie Wilmès anazuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika ziara ambayo itampeleka hadi katika mji wa Lubumbashi lengo likiwa ni kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya mataifa mawili.

Kaimu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Sophie Wilmès anayezuru nchini DRC
Kaimu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Sophie Wilmès anayezuru nchini DRC DIRK WAEM / BELGA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kinshasa na Brussels zinaonekana kuimarisha tena mahusiano yake, baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2018 na Felix Tshisekedi kuchaguliwa kuongoza nchi hiyo tajiri yenye rasilimali, barani Afrika.

Bi. Wilmès ameambatana na Mawaziri kadha katika ziara hiyo, ambayo siku ya Alhamisi, alikutana na rais Felix Tshisekedi jijini Kinshasa, na wawili hao kuzungumzia uhusiano kati ya nchi hizo mbili kibiashara na kiusalama.

Rais Tshisekedi, baada ya kuingia madarakani, alizuru Ubelgiji, nchi ambayo ilikuwa koloni ya DRC, na kuomba kurejeshwa kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2018, Ubelgiji, ilimrudisha nyumbani balozi wake na kuinyima fedha nchi hiyo kuandaa uchaguzi huo,  lakini mambo yamebadilika, baada ya Brussels kurejesha balozi wake jijini Kinshasa na hivi karibuni, kufungua ubalozi mdogo mjini Lubumbashi.

Mwaka 2019, Waziri wa Mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders alitangaza kuwa baada ya Uchaguzi nchini DRC na serikali mpya kuanza kufanya mageuzi mbalimbali, uhusiano kati yake na Kinshasa, unarudi kama kawaida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.