Jenerali anayechukuliwa kama muhusika mkuu wa mashambulizi nchini Ethiopia auawa
Mkuu wa usalama katika Jimbo la Amhara, Jenerali Asaminew Tsige, ambaye anachukuliwa kama muhusika mkuu wa mashambulizi mawili siku ya Jumamosi, ameuawa Jumatatu wiki hii, kwa mujibu wa televisheni ya EBC, ilio karibu na utawala.
Imechapishwa:
Mashambulizi hayo yaliyogharimu maisha ya Mkuu wa jeshi ya nchi hiyo na maafisa kadhaa waandamizi katika jimbo la Amhara.
Kituo cha televisheni cha EBC kimebaini katika katika muhtasari wa habari kwamba Jenerali Asaminew, "ambaye alikuwa mafichoni tangu jaribio la mapinduzi lililotibuliwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita, alipigwa risasi katika eneo la Zenzelma huko Bahir Dar" , mji wa kaskazini magharibi mwa Ethiopia.
Jenerali Saare na Gavana wa Amhara, bwana Ambachew Mekonnen ambaye pia aliuawa Jumamosi, walikuwa wakionekana kama washirika wakubwa wa Waziri Mkuu Abiy.
Bendera zinapepea nusu mlingoti baada ya serikali kutangaza kuwa siku ya maombolezo.
Brigedia Jenerali Asaminew Tsige, ambaye alikuwa ni miongoni mwa maafisa wa juu wa jeshi walioachiwa huru mwanzoni mwa mwaka jana baada ya serikali iliyopita kuwaachia wafungwa wa kisiasa kutokana na msukumo kutoka kwa umma, alikuwa ni mkuu wa usalama wa jimbo la Amhara.