Pata taarifa kuu
SOMALIA-HAKI-USALAMA

Somalia yamuua Abdulkadir Abukar Shaa'ir

Somalia imemua mmoja wa wapiganaji wakuu wa kundi la kigaidi la Al Shabab, Abdulkadir Abukar Shaa'ir, ambaye alipigwa risasi na kikosi maalum cha jeshi Desemba 24 asubuhi.

Mlipuko mpya ikitokea nje ya Hoteli ya Weheliye Mogadishu Machi 22, 2018.
Mlipuko mpya ikitokea nje ya Hoteli ya Weheliye Mogadishu Machi 22, 2018. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Abdulkadir Abukar Shaa'ir alikuwa mpiganaji mkuu wa kundi la Al Shabab na alihusika katika mashambulizi matatu ya mabomu katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mtaalamu, Abdulkadir Abukar Shaa'ir alikuwa na wasifu wa kipekee. Abdulkadir Abubakar Shaa'ir alikuwa na umri wa miaka 41, na alikuwa mzee kuliko magaidi wengi waliohusika na mashambulizi ya mabomu. Mtu huyo pia alisoma na kuhitimu elimu ya juu.

Alihusika katika shambulizi la mwezi Machi 2017 dhidi ya Hoteli ya Weheliye katika mji mkuu wa Mogadishu, shambulizi ambalo liligharimu maisha ya watu kumi. Wiki tatu baadaye, aliendesha gari lililokuwa limejaa vilipuzi na kulipuka mbele ya mgahawa ulio karibu na Wizara ya Michezo, na kuua watu tisa. Pia alihusika katika shambulizi dhidi ya baa moja linalomilikiwa na raia wa Italia Mei 2017, na kuua watu saba.

Abdulkadir Abukar Shaa'ir alikamatwa muda mfupi baada ya operesheni hiyo akiwa akiendesha gari lililobeba vilipuzi. Alipofikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, alihukumiwa kifo Desemba 6. Kikosi maalum kilimwua, na kuifanya Somalia moja ya mataifa machache Kusini mwa Jangwa la Sahara ambalo bado linatekeleza adhabu ya kifo.

Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, nchi 20 za Kusini mwa Jangwa la Sahara zimefuta adhabu ya kifo na idadi ya mauaji imepungua. Hata hivyo, Somalia inaongoza kwa kutekeleza adhabu ya kifo ambapo watu 24 walinyongwa mwaka jana.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.