Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-UGAIDI

Watu saba wauawa baada ya milipuko miwili ya bomu mjini Mogadishu

Watu saba wameuawa mjini Mogadishu nchini Somalia, baada ya kutokea kwa milipuko miwili ya bomu iliyokuwa imetegwa ndani ya magari madogo karibu na Ikulu ya rais.

Shambulizi la bomu mjini Mogadishu
Shambulizi la bomu mjini Mogadishu REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi Ibrahim Mohamed amesema watu wengine zaidi ya 10 wamejeruhiwa katika shambulizi hilo lililotokea siku ya Jumamosi.

Wafanyikazi watatu wa kituo cha Televsheni cha Universal ni miongoni mwa wale waliopoteza maisha.

Mashambulizi haya yamekuwa yakishtumiwa kutekelezwa na kundi la kigaidi al Al Shabab.

Kundi la Al Shabab limekuwa likilenga kuiondoa madarakani, serikali ya Mogadishu inayotambuliwa Kimataifa licha ya kuondolewa katika jiji hilo mwaka 2011.

Shambulizi baya zaidi, lilitokea mwezi Oktoba ambapo watu 512 walipoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.