Pata taarifa kuu
SOMALI-SIASA-USALAMA

Rais wa Somalia akabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed anayefahamika kwa jina la Farmajo, anakabiliwa na hali ngumu ya kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki linalokumbwa na mdororo wa usalama baada ya wabunge kadhaa kutokuwa na imani naye.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed.
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed. REUTERS/Ismail Taxta
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumapili usiku wabunge 92 kati ya 275 wanaomba kupigwa kura ya kutokuwa na imani naye.

"Rais amekiuka katiba kwa kukubali kushiriki katika mkataba wa siri na nchi za kigeni", yaani Ethiopia na Eritrea, kwa "kuratibu kwa pamoja bandari " na "kuunganisha nchi hii na Eritrea na Ethiopia ", kulingana na nakala iliyowasilishwa na wabunge hao kwa Spika wa Bunge.

Mapema mwezi Novemba, Rais Farmajo alikutana na wenzake kutoka Eritrea Issaias na Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmed Abiy katika mkutano Kaskazini mwa Ethiopia wenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kikanda kiuchumi kati ya nchi zao baada ya miaka kadhaa ya uhasama.

Ili kura hiyo ipitishwe, kunahitajika theluthi mbili ya wabunge 275 sawa na wabunge184, idadi ambayo ni vigumu kuifikia kwa mujibu wa waangalizi kutoka Somalia.

Nakala hiyo iliwailishwa na kukubaliwa siku ya Jumapili jioni na Spika wa Bunge, Mohamed Mursal Sheik Abdirahman, lakini siku ya Jumatatu, Manaibu wawili wa Spika wa Bunge walikosoa uamuzi huo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.

Somalia inaendelea kukumbwa na mdororo wa usalama kufuatia mashambulizi ya kila kukicha ya Al Shabab.

"Spika wa Bunge aliharakia kupokea nakala hiyo, hali ambayo inatupelekea kufikiri kuwa ana hasira kwa sababu nyingine," amesema Abdiweli Ibrahim Mudey, Naibu wa kwanza wa Spika wa Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.