Pata taarifa kuu
LIBERIA-RWANDA-MO IBRAHIM

Ellen Jonhson Serleaf ashinda tuzo ya Mo Ibrahim

Rais mstaafu wa Liberia Bi: Ellen Jonhson Serleaf ameshinda tuzo ya Mo Ibrahim jijini Kigali baada ya kukidhi vigezo ikiwemo kupigania amani.

Raisi wa zamani wa liberia Ellen Jonhson Serleaf
Raisi wa zamani wa liberia Ellen Jonhson Serleaf REUTERS/Thierry Gouegnon/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Akibubujikwa machozi ya furaha, Bi Sirleaf amesema kwamba ''Nina imani kuwa, wanawake na wasichana watafuata nyayo zangu na kuiga yale niliyoyafanya, kwani palipotoka mwanamke wa kwanza ndipo na wapili hutokea na hata wa tatu''.

Licha ya hayo Miongoni mwa watu wanaofuatilia tuzo hizo wanadai kuwa Bi Sirleaf hakidhi tuzo hiyo kwa madai kwamba Bi: Ellen Johnson Sirleaf alisaliti chama chake katika uchaguzi uliopita hatua iliyopelekea kushindwa kwa chama hicho na kadhalika.

Licha ya wakosoaji bado watu wengi wamempongeza huku taasisi ya Mo Ibrahim, ikitupilia mbali shutuma zinazotolewa dhidi ya mshindi huyo kuwa hazina mantiki. Kama alivyoeleza rais mstaafu wa Ireland Merry Robinson mmoja wa viongozi wa taasisi ya Mo Ibrahim.

 Sifikirii hivyo kwa sababu hilo ni swala la ndani ya Liberia , tunaangalia kile alichokifanya kama rais wa Liberia kwa mihula yake miwili, baada ya kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, Liberia ni nchi iliyoendelea kama inavyooneshwa na Mo Ibrahim, hayo yote tunayajua na ni mtu anayestahili nafasi hiyo.

Bi: Sirleaf amekuwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya tano amechukua tuzo hiyo baada ya wenzake sita ambao nao walitunzwa na taasisi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.