Pata taarifa kuu
Liberia

Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia aapishwa kutumikia wadhifa wa urais kwa awamu ya pili

Mshindi wa Tuzo la amani la Nobel na Raisi mteule wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ameapishwa hii leo kushika awamu nyingine ya uongozi katika serikali ya liberia baada ya kumbwaga mpinzani wake katika kinyanganyiro cha uchaguzi. 

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf
Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf REUTERS/Finbarr O'Reilly
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hizo za kiapo zimehudhuriwa na mamia ya wananchi na wakuu wa nchi mbalimbali akiwemo waziri mkuu wa marekani Hilary Clinton ambaye alisema raisi Sirleaf amefanya juhudi kubwa katika kuijenga upya nchi yake.

Raisi Ellen Sirleaf ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kwa demokrasia barani Afrika na amefanikiwa kuwatuliza wapinzani wake ambapo tayari upinzani umekubali ushindi wa sir leaf siku ya jumapili baada ya majuma kadhaa ya mazungumzo baada ya kipindi kigumu cha uchaguzi.
 

Sirleaf ameinua uwekezaji wa zaidi ya euro milioni 11 katika sekta za madini, kilimo misitu,ugunduzi,na ameshinda zaidi ya dola bilioni nne katika msamaha wa madeni.
 

Lakini ukosefu wa ajira na kukithiri kwa umasikini bado ni changamoto nchini humo,ambapo raisi sirleaf ameahidi katika mwaka ujao wa serikali ataboresha mafunzo ya ufundi kwa vijana kwakuwa vijana wengi hawana ujuzi wa kutosha kuajiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.