Pata taarifa kuu
MSUBIJI-USALAMA

Maporomoko ya mlima wa takataka yaua zaidi ya watu 17 Msumbiji

Watu wasiopungua 17 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya kuangukiwa na mlima wa taka siku ya Jumatatu asubuhi katika kitongoji cha watu wenye maisha duni cha Maputo, mji mkuu wa Msumbiji.

Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, ambapo watu 17 walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na Mlima wa taka.
Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, ambapo watu 17 walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na Mlima wa taka. DR
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa VOA Afrique, tukio hilo lilitokea usiku baada ya mvua kali ambazo zilisababisha kuanguka kwa mlima huo wa taka. Nyumba saba ziliharibika vibaya baada ya kuangukiwa na mlima huo.

"Hadi sasa, miili 17 imegunduliwa, na tuna hofu kuwa huenda tukapata miili minginei," Despedita Rita, mmoaj wa maafisa katika kitongoji hicho ameambia waandishi wa habari.

Mizozo ya ardhi katika nchi nyingi barani Afrika inapelekea watu kujenga sehemu pasio stahili na kusababisha madhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.