Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA

Serikali ya Cote d'Ivoire kutafutia ufumbuzi madai ya askari wanaogoma

Serikali ya Cote d'Ivoire, imeanza juhudi za kujaribu kuzima mgomo wa wanajeshi wa vikosi maalumu nchini humo, wakati huu hofu ya kuenea kwa vurugu mpya ikizidi kutanda baada ya majuma kadhaa ya maandamano ya vyombo vya usalama kushinikiza nyongeza ya mshahara.

Wanajeshi walioasi wakisalimiana hivi karibuni kwenye mji wa Bouake, Cote d'Ivoire.
Wanajeshi walioasi wakisalimiana hivi karibuni kwenye mji wa Bouake, Cote d'Ivoire. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Habari Bruno Kone amelazimika kufanya mazungumzo na wawakilishi wa wanajeshi hao kujaribu kupata suluhu ili kunusuru kile ambacho wadadisi wa mambo wanasema ni uasi ndani ya jeshi.

Mgomo wa wanajeshi hawa wa kikosi maalumu, umekuja ikiwa ni majuma machache tu yamepita, toka kushuhudiwa kwa uasi kama huo kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo wanajeshi walioshiriki kumuweka madarakani rais Ouattara walitaka kupandishwa vyeo na kulipwa marupurupu yao.

Hali ya sintofahamu imeendelea kushuhudia katika maeneo mbalimbali ya nci hiyo baada ya askari hao kuingia mitaani na kufyatua risasi hewani wakidai walipwe marupurupu yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.