Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KIFO

Serikali ya DRC yaandaa mazishi ya heshima kwa Tshisekedi

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema kuwa itahakikisha kuwa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi anapata mazishi ya heshima.

Joseph Kabila ameomba serikali ya DR Congo kuandaa mazishi ya Etienne Tshisekedi, kwa ushirikiano na familia ya marehemu.
Joseph Kabila ameomba serikali ya DR Congo kuandaa mazishi ya Etienne Tshisekedi, kwa ushirikiano na familia ya marehemu. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali Lambert Mende ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, Kamati maalum imeundwa kushughulikia mazishi ya mwanasiasa huyo.

Tshisekedi alifariki dunia wiki hii akiwa jijini Brussels nchini Ubelgiji, alikokuwa amekwenda kutibiwa.

Raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameendelea kuomboleza na kumlilia kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo, Etienne Tshisekedi, ambaye amefariki Jumanne wiki hii jijini Brussels alipokua akipatiwa matibabu katika hospitali ya St, Elizabeth nchini Ubelgiji.

Hayo yakijiri vijana wanaojumuika katika kundi la wanaharakati wanaotetea demokrasia na utawala bora, Filimbi, wamesema watajidhatiti kufanikisha jitihada alizoonyesha kiongozi huyo katika kuimarisha demokrasia.

Katika hatua nyingine mmoja wa waasisi wa chama cha UDPS Albert Moleka, amesema pamoja na kuondokewa kwa kiongozi huyo watajipanga kukiimarisha zaidi chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.