Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KIFO

Kifo cha Tshisekedi: Rambirambi zaendelea kumiminika kwenye makao makuu ya UDPS

Raia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameendelea kuomboleza na kumlilia kiongozi mkongwe wa upinzani nchini humo, Etienne Tshisekedi, ambaye amefariki Jumanne wiki hii jijini Brussels alipokua akipatiwa matibabu katika hospitali ya St, Elizabeth nchini Ubelgiji.

Nje ya makao makuu ya chama cha UDPS katika mji wa Kananga, Alhamisi, Februari 2, 2017.
Nje ya makao makuu ya chama cha UDPS katika mji wa Kananga, Alhamisi, Februari 2, 2017. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Rambirambi zimeendelea kumiminika nchini kote baada ya kifo cha kiongozi huyo wa upinzani. Katika mji wa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini pia katika mkoa alikozaliwa wa wa Kasai ya Kati. Katika mji wa Kananga, katika makao makuu ya chama chake, UDPS, maelfu ya wafuasi wamekusanyika.

Wakati huo huo vijana wanaojumuika katika kundi la wanaharakati wanaotetea demokrasia na utawala bora, Filimbi, wamesema watajidhatiti kufanikisha jitihada alizoonyesha kiongozi huyo katika kuimarisha demokrasia.

Katika hatua nyingine mmoja wa waasisi wa chama cha UDPS Albert Moleka, amesema pamoja na kuondokewa kwa kiongozi huyo watajipanga kukiimarisha zaidi chama hicho.

Hayo yakijiri fujo zimeshuhudiwa kwa mara nyingine nje ya ofisi za chama kikuu cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, UDPS, ambapo polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa mwanasiasa Etienne Tshisekedi, ambao wanaendelea kufurika jijini Kinshasa kuomboleza kifo chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.