Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KIFO

Wasifu wa mwanasiasa mkongwe wa upinzani nchini DRC Etienne Tshisekedi

Etienne Tshisekedi wa Mulumba alizaliwa Desemba 14, 1932 mjini Kananga, Jimbo la Kasai ya Kati, Kasai Occidental wakati huo, mji wa Kananga uliitwa Luluabourg wakati nchi ya DR Congo ikijulikana kama Congo-Belge.

Etienne Tshisekedi en meeting à Kinshasa, le 31 juillet 2016.
Etienne Tshisekedi en meeting à Kinshasa, le 31 juillet 2016. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Tshisekedi wa Mulumba aliingia katika ulimwengu wa siasa akiwa na umri wa miaka 29, punde baada ya kupata shahada yake ya kwanza baada ya kuhitimu masomo ya Sheria.

Tshisekedi alianza kuvutiwa na siasa baada ya kujiunga na vyama vya Vijana walioshawishika na siasa punde baada ya nchi hiyo kupata Uhuru kutoka kwa Ubelgiji, aliteuliwa katika jopo la maafisa wakuu ambao Mobutu aliwateua kuendesha serikali, ambayo Januari 1961 alikuwa bado mwanafunzi wakati kanali wa jeshi, Joseph Desire Mobutu, alipotwaa madaraka na kutangaza kumpindua waziri mkuu maarufu wa zamani, Patrice Lumumba na rais Joseph Kasa-Vubu.

Baada ya Mobutu kufanya mapinduzi Novemba 1965, Tshisekedi alihudumu kama waziri wa mambo ya ndani, sheria na mipango ya taifa, na alikuwa katibu wa kwanza wa chama cha Mobutu cha MPR.

Alichaguliwa tena mbunge 1970, lakini baadaye akatofautiana na Mobutu. Etienne Tshisekedi pamoja na wabunge wengine walianza kutofautiana na Mobutu baada ya kumuandikia barua ya wazi kupinga utawala wa kifisadi na kidikteta kama walivyosema kupitia barua hiyo. Aliwekwa gerezani na kuachiwa huru 1982, mwaka ambao aliunda chama cha UDPS, ambachoi baadaye kilikuja kuwa chama kikuu cha Upinzani baada ya Mobutu kuondosha marufuku dhidi ya vyama vya siasa miaka ya 1990.

Akipigania mageuzi ya demokrasia huku akionyesha kuupinga utawala wa Mobutu, Tshisekedi alichaguliwa kuwa waziri mkuu Agosti 1992, lakini Mobutu akamtimua siku tatu baadaye. Tshisekedi hata hivyo aliendelea kushikilia nafasi hiyo kwa miezi saba, ingawa serikali aliyoiongoza haikutambuliwa na Mobutu.

Baada ya Mobutu kupinduliwa mwaka 1997 katika mapinduzi yaliyoongozwa na Laurent Desire Kabila, babake rais wa sasa, Joseph Kabila, Tshisekedi kwa haraka aligeuka kuwa mpinzani wa utawala mpya, msimamo ambao uliendelea baada ya Laurent Kabila kuuliwa mwaka 2001 na baadaye mtoto wake, Joseph Kabila, kuingia madarakani.

Tshisekedi alisimama kidete kuupinga utawala wa Mobutu Sese Seko ambaye aliitawala DRC, wakati huo ikijulikana kama Zaire, alikuwa mpinzani wake kwa miaka mingi kabla ya Mobutu kupinduliwa.

Baadaye lakini Tshisekedi aligeuka na kuwa mpinzani mkubwa wa Mobutu. Alikuwa pia mpinzani mashuhuri wa rais Laurent Kabila, aliyetwaa madaraka mnamo mwaka 1997, na mtoto wake rais wa sasa Joseph Kabila, ambaye ameiongoza Congo tangu mwaka 2001.

Tshisekedi, kiongozi ambaye hakuonekana sana hadharani kwa kipindi kirefu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na afya yake kuzorota, alikuwa amesafiri kwenda Brussels siku ya Jumanne Januari 26, wakati ambapo Congo iko katika wakati muhimu sana kisiasa.

Muungano wa upinzani wa Rassemblement aliokuwa akiuongoza unafanya mashauriano juu ya hatua za kuchukuliwa katika mkataba wa kugawana madaraka uliosainiwa desemba 31 mwaka uliopita kuepusha machafuko mapya baada ya rais Kabila kukataa kuondoka madarakani muhula wake ulipokamilika mwaka uliopita.

Mmoja kati ya watoto watano wa Tshisekedi, Felix Tshisekedi, ana matumaini ya kutangazwa waziri mkuu katika serikali ya mpito kwa mujibu wa makubaliano ya hivi karibuni chini ya upatanishi wa baraza la maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Cenco.

Wafuasi wa upinzani wakiwa na picha ya kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi, picha ya hivi karibuni.
Wafuasi wa upinzani wakiwa na picha ya kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC, Etienne Tshisekedi, picha ya hivi karibuni. DR

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.