Pata taarifa kuu
SOMALIA

Watu 10 wauawa baada ya Al Shabab kushambulia Hoteli maarufu mjini Mogadishu

Watu 10 wameuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya kutokea kwa shambulizi la bomu mjini Mogadishu nchini Somalia.

Shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia
Shambulizi la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Mogadishu imethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo katika hoteli moja inayofahamika kama Dayah, ambayo pia inawapa hifadhi watu mashuhuri kama wabunge.

Polisi wanasema, shambulizi hilo lilitokea baada ya magari mawili madogo yaliyokuwa yamebeba mabomu na vilipuzi kulipuka mbele ya hoteli hiyo.

Waziri wa usalama nchini humo Abdirizak Omar Mohamed amesema washambulizi wanne waliotekeleza waliokuwa ndani ya magari hayo wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Aidha, polisi inasema kuwa imefanikiwa kudhibiti jengo hilo na kuwaokoa watu wengine waliokuwa ndani ya hoteli hiyo ambayo inakaribia na makaazi ya rais.

Kundi la kigaidi la Al Shabab limesema ndilo lililotekeleza shambulizi hilo.

Hii ndio mara ya kwanza kwa mwaka 2017 kwa Al Shabab kutekeleza shambulizi katika hoteli maarufu mjini Mogadishu.

Mwezi Desemba mwaka 2016, zaidi ya watu 20 walipoteza maisha baada ya Lori lililokuwa limebeba mabomu na vilipuzi kulipuka karibu na kambi ya kijeshi mjini Mogadishu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.