Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB

Al Shabab yaendelea na mashambulizi yake nchini Somalia

Kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia linadhibiti mji Goofgaduud Kilomita zaidi ya mia mbili kutoka mji mkuu Mogadishu. Taarifa hii imethibitishwa na baadhi ya maafisa wa usalama nchini Somalia.

Askari wa Somalia akipiga doria katika mji wa  Afgoye,kusini mwa nchi, baada ya shambulizi la kujitoa mhanga lililowaua watu Oktoba 19, 2016.
Askari wa Somalia akipiga doria katika mji wa Afgoye,kusini mwa nchi, baada ya shambulizi la kujitoa mhanga lililowaua watu Oktoba 19, 2016. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Operesheni za Al Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab amethibitisha kudhibitiwa kwa mji huo na kuongeza kuwa, wanajeshi saba wa Somalia waliuawa.

Hata hivyo, Meja Hussein Edin kutoka jeshi la Somalia amesema walivamiwa na magaidi hao na kumuua mwanajeshi wao mmoja.

Kundi la Al Shabab limeendelea kutekeleza mashambulizi nchini Somalia likiwa na lengo la kudhibiti nchi hiyo.

Itakumbukwa kwamba Jumatano Oktoba 25, wapiganaji wa kundi la Islamic State walichukua udhibiti wa mji wa Qandala, mji wa ulio katika mkoa unaojitegemea wa Puntland. Ni kwa mara ya kwanza mji huu unaanguka mikononi mwa kundi la kijihadi nchini Somalia.

Huu hunda ukawa ushahidi tosha wa kusonga mbele kwa kundi la IS nchini Somalia. Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, wanamgambo wa Kiislamu hamsini walishambulia mji huo Jumatano asubuhi. Baada ya mapigano ya muda mfupi na vikosi vya usalama, washambuliaji walichukua udhibiti wa mji huu wenye wakazi 20 000 unaopatikana kaskazini mashariki mwa mkoa unaojitegemea wa Puntland.

Kwa mujibu wa afisa wa Somalia aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP, askari walikuwa wachache na walilazimika kuondoka katika mji huo. Afisa huyo amesema itakuwa ni mara ya kwanza kundi la Islamic State kudhibiti mji wa Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.