Pata taarifa kuu
GAMBIA-NIGERIA-SIASA

Nigeria kumpa hifadhi rais Yahya Jammeh

Ikiwa zimesalia siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kukaa madarakani kama rais kulingana na katiba, rais wa Gambia Yahaya Jammeh ameendelea kupinga kuondoka mamlakani kabla ya uamuzu wa mahakama ya juu nchini humo, ambayo hivi karibuni ilitangaza kuahirisha kusikiliza kesi kuhusu uchaguzi wa mwezi Desemba hadi mwezi Mei.

Yahya Jammeh, rais wa Gambia aliyeshindwa katika uchaguzi lakini amekataa katu katu kuondoka mamlakani.
Yahya Jammeh, rais wa Gambia aliyeshindwa katika uchaguzi lakini amekataa katu katu kuondoka mamlakani. AFP PHOTO / SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Bunge nchini Nigeria limeunga mkono mswada wa kumpatia hifadhi rais Yahya Jammeh iwapo atajiuzulu.

Wabunge hao walitumia takriban nusu saa kujadili pendekezo hilo lililowasilishwa na Fani Zoro anayesimamia kamati ya wakimbizi bungeni.

Rais Yahya Jammeh alishindwa uchaguzi mwezi Desemba, lakini anataka matokeo ya kura hiyo kufutiliwa mbali.

Baadhi ya wanachama hawakuunga mkono mapendekezo hayo wakisema kuwa wanamtambua rais Jammeh kuwa dikteta aliyechukua uongozi kupitia mapinduzi mwaka 1994 na kudai kuwa hatua kama hiyo itatuma ujumbe mbaya kwa viongozi wengine.

Hatahivyo wabunge wengi waliunga mkono wakisema itakuwa njia ya kuzuia mgogoro zaidi.

Wabunge hao wanahofu ya kutokea maafa nchini Gambia iwapo rais Jammeh ataendelea kusalia madarakani, na hali hiyo huenda ikayakumba mataifa jirani ya nchi hiyo, wamesema wabunge wa Nigeria waliokutana Alhamisi hii katika kikao chao cha kwanza baada ya kutoka likizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.