Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Maaskofu nchini DRC washinikiza kutekelezwa kwa mkataba wa kisiasa

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linakutana jijini Kinshasa kutathmini hatua iliyopigwa kuhakikisha mkataba wa kisiasa uliokubaliwa mwezi Desemba mwaka 2016, unaanza kutekelezwa kikamilifu.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC Kushoto ni Kadinali Laurent Monsengwo Pasinya, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu nchini humo
Maaskofu wa Kanisa Katoliki DRC Kushoto ni Kadinali Laurent Monsengwo Pasinya, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu nchini humo RFI
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unafanyika wakati huu kukiwa na mvutano kati ya wanasiasa wa upinzani na serikali kuhusu namna ya kugawana madaraka.

Nao muungano wa vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, umezindua mpango maalum unaonekana kama hatua ya kwanza kuelekea uteuzi wa mtu atakayemrithi rais Joseph Kabila, baada ya muda wake kumalizika kufikia mwisho wa mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Msemaji wa wanasiasa wa upinzani wa G7 Christophe Lutundula amesema wameendelea kutoa wito kwa Muungano wa wanasiasa wanaopinga mkataba huo wa kisiasa kuukubali.

Umoja wa Mataifa pia umewataka wadau wa kisiasa nchini humo kuheshimu makubaliano hayo ili mwafaka upatikane katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Upinzani unaoongozwa na Ettiene Tshisekedi, kwa mujibu wa mkataba huo, unatoa nafasi ya Waziri Mkuu ambayo kwa sasa anashikiliwa na Samy Badibanga, ambaye ameonekana kupinga mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.