Pata taarifa kuu
NIGRIA-BOKO HARAM-USALAMA

Shekau: Bado tupo Sambisa

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, amerusha hewani Alhamisi hii Desemba 29 video mpya ambapo anakanusha madai ya serikali ya Nigeria kwamba kundi la wanajihadi la Boko Haram lilitimuliwa katika msitu wa Sambisa, moja ya ngome yake ya mwisho kaskazini mwa nchi hiyo.

Picha iliyonaswa katika video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, Aprili 13, 2014.
Picha iliyonaswa katika video ya propaganda ya Boko Haram ikimuonyesha kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, Aprili 13, 2014. AFP PHOTO / BOKO HARAM
Matangazo ya kibiashara

"Sisi ni salama, hatujatimuliwa mahali popote pale. Na mbinu pamoja na mikakati haviwezi kutenganisha msimamo wetu isipokuwa Mungu akitaka," amesema Shekau, akiwa amezungukwa na wapiganaji waliojificha nyuso zao huku wakishikilia silaha, katika video ya dakika ya 25.

Wiki iliyopita, Rais wa Nigeria alibaini kuwa jeshi la Nigeria liliwatimu wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika ngome yao ya mwisho ya msitu Sambisa.

Boko Haram imekua ikitekeleza mashambulizi ya kujitoa muhanga kaskazini-mashariki mwa Nigeria na nchi jirani ya Niger na Cameroon.

Kulingana na makadirio, kundi la la Boko Haram liliua zaidi ya watu 15,000 wna kusababisha watu zaidi ya milioni mbili kuyahama makaazi yao kwa uasi unaodumu sasa miaka saba katika ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.