Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-SHEKAU

Nigeria: Abubakar Shekau aonekana dhaifu katika video mpya

Kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, ameonekana Alhamisi hii katika video mpya, akikanusha uvumi kuhusu kifo chake lakini ameonekana dhaifu na kutangaza kwamba mwisho wake unakaribia.

Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram.
Aboubakar Shekau, kiongozi wa kundi la Boko Haram. Fuente: YouTube
Matangazo ya kibiashara

"Kwangu mimi, mwisho unakaribia," amesema Shekau, huku akikunja uso, katika video mpya, ambayo haikutengenezwa ubora zaidi, iliyorushwa kwenye Youtube. Haijulikani wapi na wakati gani video ilitengenezwa, na Jeshi la Nigeria limesema limeanza kuchunguza uhalali wa video hiyo.

"Mwenyezi Mungu atulinde na maovu (...) Namshukuru Muumba wangu," Shekau ameendelea, huku akianza kusema kwa sauti ya chini, kwa lugha ya Kihausa na Kiarabu, kwa sauti ya chini ambayo si kawaida yake. Alitangaza mwezi Machi 2015 kuwa kundi lake linajiunga na kundi Islamic State (IS).

Tofauti na video awali za kundi la Kiislam la Nigeria, ziliorushwa hewani mwishoni mwa mwaka 2014 na mapema mwaka 2015, ambazo zilikua na picha zenye ubora mzuri, na zilitengenezwa kwa utaalamu, na ambazo zinafanana na zile za kundi la Islamic State, video hii mpya imetengenezwa vibaya.

Shekau hazungumzii kundi la IS, na anatumia jina asili la Boko Haram, "Jama'atu Ahlis Sunna Lidda'awati wal-Jihad" - "watu waliojikubalisha kueneza mafundisho ya nabii na jihad".

Aidha, video haikurushwa hewani kwenye moja ya akaunti ya Twitter yenye uhusiano na washirika wa kundi la Islamic State pamoja na makundi mengine ya wanajihadi, kama ilivyokuwa hapo awali.

"Wakati unapoangalia video hii mpya ya Shekau, ujumbe uko wazi: amekwisha," chanzo cha kijeshi kimejibu katika mji wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno (kaskazini).

"Ili gaidi huyu mwenye kiburi na majivuno aongee kwa sauti ya chini na yenye huzuni, hii inaonyesha kwamba ameshindwa na yuko katika hatua ya kuangamia," chanzo hicho kimeongeza.

"Hii ni video ya kuaga. Anawaambia wapiganaji wake waweze kusema kwaheri kwa kundi la Islamic State sawa na kumaanisha waweke silaha chini (...) Anajua kwamba kutokana na kusonga mbele kwa jeshi la Nigeria, askari wetu watamkamata hivi karibuni. "

Jeshi, hata hivyo, limetoa taarifa ambapo linatangaza kuwa na "ufahamu wa video hiyo(...) ambayo imeanza kufanyiwa uchunguzi" ili "kuhakikisha uhalali wake."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.