Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI

Nigeria: 21 wauawa na 91 wajeruhiwa katika mashambulizi

Watu zaidi ya 20 wameuawa katika mashambulizi zaidi ya matatu yalioendeshwa Jumapili usiku na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram katika mji wa Maiduguri, nchini Nigeria.

Askari wa Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram, Novemba 8, 2015.
Askari wa Nigeria wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Boko Haram, Novemba 8, 2015. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Watu wengi wameuawa baada ya kijiji cha Dawari na vitongoji vyake kushambuliwa na watu waliokua wamejihami kwa bunduki Jumapili usiku.

Hata hivyo jeshi limebaini kwamba liliwaua wapiganaji 10 walioshukiwa kuwa washambuliaji wa kujitoa mhanga.

Mapema Jumatatu, mwanamke amejilipua wakati watu walipokuwa wakijiandaa kuingia Msikitini.

Chanzo cha polisi kimesema katika muda wa saa 24, mashambulio manne ya kujitoa mhanga yametekelzwa, na yote yaliendeshwa na wanawake.

Mji wa Maiduguri wakati mmoja ulichukuliwa kuwa ngome kuu ya wapiganaji wa Boko Haram.

Hivi karibuni Boko Haram imezidisha mashambulio ya kujitoa mhanga katika mji wa Maiduguri na maeneo mengine kaskazini mwa Nigeria.

Kundi hili la Boko Haram linanatumia wanawake vijana wa umri mdogo kwa kutekeleza mashambulizi ya kujitoa mhanga.

Hivi karibuni rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alipongeza majeshi yake na kusema kuwa yalikuwa yamewashinda wapiganaji wa Boko Haram, huku akibaini kwamba wapiganaji wa kundi hilo hawawezi tena kuendesha mashambulizi katika maeneo yenye wakazi wengi, hususan mijini na katika kambi za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.