Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Watu zaidi ya 40 wafariki Nigeria

Idadi isiyojulikana ya watu wamepoteza maisha Kusini mwa Nigeria baada ya kutokea kwa mlipuko katika kiwanda cha kuzalisha gesi.

Kiwanda cha Ajaokuta Steel Company, kilichopuuzwa kwa zaidi ya miaka 30, Nigeria.
Kiwanda cha Ajaokuta Steel Company, kilichopuuzwa kwa zaidi ya miaka 30, Nigeria. RFI/Awwal
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema mlipuko huo ulitokea wakati Lori la gesi ya kupikia lilipokuwa linaingiza gesi katika kiwanda hicho katika jimbo la Anambra.

Inahofiwa kuwa watu waliopoteza maisha ni kati ya 35 na 100, na watu hao wanaripotiwa kuwa ni wafanyikazi wa kiwanda hicho na majirani.

Polisi katika jimbo hilo wamethibitisha mkasa huu lakini hawajatoa idadi kamili ya watu waliopoteza maisha.

Gazeti la Vanguard linaripoti kuwa, moto ulikuwa mkubwa sana na uliwachukua maafisa wa Zima Moto muda mrefu kuuzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.