Pata taarifa kuu
NIGERIA-SIASA

Nigeria baraza jipya la mawaziri latangazwa

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari hatimaye ametangaza Baraza lake la mawaziri thelathini na sita pamoja na manaibu waziri, miezi zaidi ya mitano baada ya kukabidhiwa hatamu za uongozi kufuatia ushinda wa uchaguzi wa urais nchini humo.

Akimzungukwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (katikati), mawaziri 36 walioteuliwa wameapa katika mji wa Abuja, Novemba 11 2015.
Akimzungukwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (katikati), mawaziri 36 walioteuliwa wameapa katika mji wa Abuja, Novemba 11 2015. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wizara muhimu, Wizara ya Fedha imepewa mwanauchumi Kemi Adeosun, aliyesomea nchini Uingereza na ambaye wakati mmoja alihudumu kama kamishna wa fedha katika jimbo la Ogun wakati ambapo Jenerali mstaafu Mansur Dan ameteuliwa kuwa wazira wa Ulinzi.

Mwanasiasa mkongwe ambaye pia ni mkulima Audu Ogbe ameteuliwa waziri wa kilimo.

Wachambuzi wanasema wizara ambazo zitakuwa na kibarua kigumu nchini humo, ni pamoja na wizara ya ulinzi, wakati huu nchi hiyo ikikabiliana na kundi la kigaidi, lakini pia wizara ya ujenzi na makazi, kufwatia mzozo wa umeme, nchini humo, na hali kadhalika wizara ya uchumi kufwatia ufuajaji wa mali ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.