Pata taarifa kuu
NIGERIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Nigeria: watu 30 wauawa katika shambulizi Yola

Shambulizi la kigaidi katika mji wa Yola nchini Nigeria umesababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Watu waliokolewa kutoka mikononi mwa Boko Haram katika kambi ya Yola Nigeria, Mei 3, 2015..
Watu waliokolewa kutoka mikononi mwa Boko Haram katika kambi ya Yola Nigeria, Mei 3, 2015.. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea katika soko lilolokuwa na watu wengi katika mji huo wa Yola Jumanne jioni wiki hii.

Shambulizi hili linakuja siku chache tu baada ya rais Mohamadu Buhari kuzuru mji huo siku ya Jumamosi wiki iliyopita na kuwaambia wenyeji kuwa kundi la Boko Haram linashindwa.

Mji huo ambao umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara mwaka huu upo katika jimbo la Adamawa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la Msalaba mwekundu linasema zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa na huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.