Pata taarifa kuu
NIGERIA-UNICEF-BOKO HARAM-USALAMA

Unicef: Boko Haram yazuia watoto milioni moja kwenda shule

Machafuko yanayoendeshwa na kundi la kiislam la Boko Haram yanazuia watoto zaidi ya milioni moja kwenda shule, shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto (UNICEF) lilitangaza Ijumaa wiki iliyopita, likibainisha kuwa ukosefu wa elimu unakuza msimamo mkali wa kidini nchini Nigeria na nchi jirani.

Watoto karibu na kibanda kiliojengwa kwa hema za UNICEF ambacho kimewekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Assaga kusini mashariki mwa Niger, Septemba 16, 2015.
Watoto karibu na kibanda kiliojengwa kwa hema za UNICEF ambacho kimewekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Assaga kusini mashariki mwa Niger, Septemba 16, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya shule 2,000 zimefungwa nchini Nigeria, Cameroon, Chad na Niger, nchi nne ambazo zinaendelea kuathirika na mashambulizi ya kundi hilo, na mamia ya taasisi nyingine zilishambuliwa, ziliporwa au kuchomwa moto na wapiganaji wa kundi la Boko Haram, kwa mujibu wa UNICEF.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alilipa jeshi hadi mwisho wa mwaka huu kuwa liwe limekomesha vurugu za kundi hilo la Boko Haram. Lakini hata kama ushindi utapatikana, wataalam wanasema kwamba serikali itakumbwa na machafuko ya kijamii kutokana na kutokwenda shule kwa watoto.

"Kadri watakua hawajakwenda shule, kuna hatari waendelea kukabiliwa na mateso, unyanyasaji, kutekwa nyara na kusajiliwa na makundi yenye silaha", Manuel Fontaine, Mkurugenzi wa UNICEF katika Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, amesema.

Uasi wa Boko Haram na mashambulizi ya vikosi vya usalama vimegharimu maisha ya watu 17,000 na wengine milioni 2.6 kukimbia makazi yao tangu mwaka 2009.

Shule, wanafunzi na walimu ni miongoni mwa vitu na watu viliolengwa na kundi hili la Boko Haram, ambalo jina lake linamaanisha "elimu ya Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, lugha inayozungumzwa zaidi kaskazini mwa Nigeria. Lengo la kundi hili ni kuanzisha taifa huru la Kiislam.

Utekaji nyara wa wanafunzi wasichana 276 katika mji wa Chibok (kaskazini) mwa Nigeria, Aprili 14, 2014 ulisababishwa wimbi la hasira dunia kote. Mpaka sasa wanafunzi 200 kati yao bado wanashikiliwa na Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.