Pata taarifa kuu
NIGERIA-USALAMA

Wasichana wawili wajilipua katika soko nchini Nigeria

Wasichana wawili walijilipua Jumapili hii asubuhi katika soko linalotembelewa na watu wengi la Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kuua angalau mtu mmoja na kuwajeruhi wengine 18, kwa mujibu wa takwimu za serikali.

Jeshi la Nigeria kwenye barabara ya Chibok, kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Machi 5, 2015.
Jeshi la Nigeria kwenye barabara ya Chibok, kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Machi 5, 2015. AFP PHOTO/SUNDAY AGHAEZE
Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la Borno, Kashim Shettima, alikwenda hospitali ambapo walisafirishwa watu waliojeruhiwa na alisem ambele ya waandishi wa habari kwamba mashambulizi hayo mawili yalisababisha kifo cha mtu mmoja na kuwajeruhi watu wengine 18.

Kwa mujibu wa Abdulkarim Jabo, mmoja wa wanamgambo wa kiraia katika mji mkuu wa jimbo la Borno ambaye alikua katika eneo la tukio, washambuliaji wa kujitoa mhanga walikua na umri kati ya 'miaka 7 au 8. '

"Wasichana walishuka kutoka kwenye baisikeli na kupita mbele yangu bila kuwa na wasiwasi wowote," shahidi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP.

"Nlijaribu kuzungumza na mmoja wao katika lugha ya Hausa na Kiingereza, lakini hakujibu. Nilidhani walikuwa wanamtafuta mama yao," ameeleza Bw Jabo. "Mmoja wa wasichana hao alijielekeza kwa wauzaji wa kuku na alifyatua mkanda wake uliokua umejaa vilipuzi," ameongeza Bw Jabo

Mlipuko wa pili ulitokea wakati wachuuzi wa soko hilo walikua wakitoa msaada kwa majeruhi.

"Tumewaondoa watu 17, ambao walikua wamejeruhiwa katika viwango tofauti,"alisema Bello Dambatta, kutoka shirika la uratibu wa hali za dharura la Sema.

Hakuna kundi hata moja ambalo limedai kuhusika na mashambulizi haya lakini mbinu iliyotumiwa ni ile ya kundi la Boko Haram, ambalo mara nyingi limekua likitumia wanawake na wasichana kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya raia.

Watu wasiopungua 45 waliuawa na 33 walijeruhiwa katika mashambulizi mawili ya mabomu yalitotokea siku ya Ijumaa, ambayo yaliendeshwa na wanawake wawili katika soko la Madagali, (katika jimbo la Adamawa), mji ulio karibu na karibu na msitu wa Sambisa, moja ya ngome za Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.