Pata taarifa kuu
NIGERIA-RFI-CAMEROON

Ufaransa yaitaka Cameroon kumuachia mwanahabari wa RFI, kupandishwa kizimbani.

Mwanahabari wa Radio France International, idhaa ya lugha ya hausa, Ahmed Abba, Jumatano ya Desemba 7, atapandishwa kizimbani katika mahakama ya mjini Yaunde, kujibu mashtaka ya kudaiwa kuwa na uhusiano na kundi la wapiganaji wa kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria.

Mwanahabari wa RFI, idhaa ya Hausa ya Nigeria, Ahmed Abba, ambaye anashikiliwa nchini Cameroon.
Mwanahabari wa RFI, idhaa ya Hausa ya Nigeria, Ahmed Abba, ambaye anashikiliwa nchini Cameroon. RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, ametoa wito kwa Serikali ya Cameroon, kumuachia huru mwanahabari wa Radio France International, RFI, idhaa ya lugha ya Hausa nchini Nigeria, Ahmed Abba, ambaye anashikiliwa na mamlaka nchini Cameroon kwa zaidi ya miezi 16 bila kufunguliwa mashtaka na hii leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya mjini Yaunde.

Mkurugenzi wa mashirika ya habari ya RFI na France Medias Monde, amesema kwenye taarifa yake kuwa, Abba amewekwa katika mazingira magumu kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku miezi minne iliyopita akiitumia akiwa hospitalini.

Hata hivyo mashahidi kwenye kesi hiyo wameshindw akuthibitisha ikiwa Abba alikuwa akishirikiana na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haramu nchini Nigeria.

Radio France International inasisitiza kuwa Ahmed Abba hana hatia na kueleza matumaini yake kuwa hii leo huenda akaachiwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.