Pata taarifa kuu
BURUNDI-RFI-AFP-SHERIA-HAKI

Burundi: RFI na AFP wafungua mashtaka kwa mateso aliyofanyiwa mwandishi wao

Shirika la habari la Ufaransa la AFP na RFI pamoja na mwaandishi wao nchini Burundi, Esdras Ndikumana, waliwasilisha mashataka yao Jumatatu wiki hii kuhusu mateso aliyofanyiwa mwandishi wao.

Vikosi vya usalama vya Burundi, jijini Bujumbura, Jumanne Julai 21, 2015.
Vikosi vya usalama vya Burundi, jijini Bujumbura, Jumanne Julai 21, 2015. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Agosti 2, Esdras Ndikumana alikamatwa na Idara ya Ujasusi (SNR) wakati alipokuwa akiendesha kazi yake ya uandishi katika eneo alikouliwa jenerali Adolphe Nshimirimna.

Ezdras Ndikumana alikamatwa na kupelekwa katika majengo ya Idara ya Ujasusi na kupigwa kwa zaidi ya saa mbili.

RFI na AFP waliwasilisha mara moja malalamiko kwa viongozi mbalimbali wa nchi ya Burundi. Siku kumi na moja baadaye, Rais Pierre Nkurunziza aliahidi vikwazo dhidi ya wale waliohusika. Na tangu wakati huo, hakuna kilichofanyika.

Licha ya barua kutoka kwa redio RFI na shirika la habari la Ufaransa la AFP, barua zilisalia bila majibu. Na ndio maana vyombo hivyo vya habri viliamua kufungua mashtaka kutokana na dharau hiyo.

Ni mashtaka mawili tofauti ambayo yamewasilishwa mbele ya Mwendesha mashitaka wa Mahakama Kuu mjini Bujumbura: "mashtaka mawili dhidi ya maafisa wa Idara ya Ujasusi kwa mateso aliyofanyiwa Esdras Ndikumana, mwandishi kwa RFI na AFP ".

Moja ya mashtaka hayo yamewasilishwa kwa jina la Esdras Ndikumana mwenyewe. Ezdras Ndikumana ameelezea jinsi gani alivyokamatwa kinyume cha sheria katika eneo la tukio alikouawa jenerali Adolphe Nshimirimana wilayani Kamenge wakati ambapo alikua akifanya kazi yake. Ilikuwa Agosti 2 mwaka huu. " Sababu ya kukamatwa kwangu kamwe sijafahamishwa ", amesema Esdras Ndikumana.

Ezdras Ndikumana alielezea jinsi gani alivyofanyiwa kipigo kwa muda wa saa mbili katika majengo ya Idara ya Ujasusi (SNR).

RFI na AFP pia wamefunguwa mashataka kwa kile wanachosema hawakutendewa haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.