Pata taarifa kuu
BURUNDI

Ripota wa RFI Kiswahili nchini Burundi Hassan Ruvakuki aachiwa huru kwa sababu za kiafya

Mahakama nchini Burundi jumatano hii imemwacha huru kwa muda usiojulikana Mwandishi wa Habari wa Radio Bonesha FM ya nchini humo na Ripota wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio France International Hassan Ruvakuki kwa sababu za kiafya. Mwanasheria wake Fabien Segatwa amesema hatua hii ni kwa ajili ya kumuwezesha Ruvakuki kupata matibabu kabla ya kurejea jela kwa mara nyingine kuendelea kutumikia kifungo chake.

AFP PHOTO/Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Ruvakuki alipokelewa kwa shangwe kubwa na familia yake, wanahabari, raia wa Burundi na wanaharakati ambao tangu awali wamekuwa wakipinga hukumu hiyo na kushinikiza kuachiliwa kwake.

Mara baada ya kurejea nyumbani Ruvakuki ameeleza furaha yake na kusema amefarajika baada ya kumuona mwanae wa kike aliyezaliwa wakati mwenyewe akiwa gerezani.

Ruvakuki alikamatwa mwezi Novemba mwaka jana akituhumiwa kushiriki katika kundi la uasi nchini Burundi, kundi ambalo liliendesha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali katika mkoa wa Cankuzo mpakani na Tanzania.

Ruvakuki alihukumiwa kifungo cha maisha mwezi June mwaka jana na baadaye mwezi januari mwaka huu kifungo chake kikapungua hadi miaka mitatu baada ya kukata rufaa.

Kumekuwa na maandamano ya Wanahabari jijini Bujumbura na miito ya kimataifa ili Ruvakuki aachwe huru, na Mwanasheria wake anasema wataendelea na mikakati ya kuhakikisha mteja wake anaachiwa huru kwani alikuwa akitekeleza kazi yake hivyo hana hatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.