Pata taarifa kuu
BIAFRA-NIGERIA

Amnesty: Jeshi na polisi Nigeria wanahusika na mauaji ya watu 150 wa Biafra

Shirika la kimataifa la Amnesty International, linavituhumu vikosi vya Serikali ya Nigeria kwa kuhusika na mauaji ya watu 150, wengi wakiwa waandamanaji wanaotaka eneo la Biafra kujitenga.

Waandamanaji wanaounga mkono eneo la Biafra kujitenga na Nigeria, Novemba 2015.
Waandamanaji wanaounga mkono eneo la Biafra kujitenga na Nigeria, Novemba 2015. AFP PHOTO / PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo jeshi la Nigeria pamoja na polisi nchini humo wametupilia mbali madai ya kuwa wamehusika kwenye mauaji hayo.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, amesema kuwa ripoti ya Amnesty International, ambayo si ya kwanza kutolewa na shirika hilo na kulituhumu moja kwa moja jeshi la nchi hiyo kwa kuhusika na mauaji ya raia, amesema ripoti yake inalenga kulichafua jeshi hilo na vikosi vingine vya usalama.

Polisi kwa upande wake inasema haijawahi kutumia nguvu wala kuwashambulia raia ambao wanafanya maandamano ya amani.

Amnesty inasema kuwa, wanajeshi walitumia risasi za moto bila kuwaonya raia waliokuwa wakiandamana, hasa kutoka kwenye eneo la Biafra kati ya mwezi Agosti 2015 na Agosti 2016.

Katika taarifa yake yenye kurasa 60, Amnesty iliwahoji watu 193, kurekodi video 87 na kupiga picha zaidi ya 122 vyote hivi vikifanyika kipindi ambacho polisi na wanajeshi walitumia nguvu kuwakabili waandamanaji.

Hali ya sintofahamu ya eneo hilo kutaka kujitenga na Nigeria, imeendelea kupanda miaka ya hivi karibuni, ambapo kuanzia mwaka 1967 hadi 1970 kulizuka vita kubwa ambayo ilisababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 1.

Harakati mpya zilizuka mwaka uliopita, baada ya kiongozi wa vuguvugu la Biafra Nnamdi Kanu kuzuiliwa na vyombo vya usalama, akituhumiwa kwa makosa ya uhaini na uchochezi.

Kukamatwa kwa Kanu, kulizusha maandamano ya wafuasi wake na ndio kipindi ambacho Amnesty International inadai ilituma waangalizi wake walioshuhudia polisi na wanajeshi wakitumia risasi za moto kuwatawanya.

Msemaji wa jeshi la Nigeria, Sani Usman, amesema wanaharakati wa Biafra ndio wanaofanya vurugu wakati wa maandamano yao, ambapo wamewaua polisi wa tano kwenye maandamano ya mwezi Mei ambapo wanajeshi pia walishambuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.