Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHUMI

Baraza la Seneti la Nigeria lafutilia mbali mpango wa Buhari

Maseneta wa Nigeria wamekataa mpango wa bajeti wa Rais Muhammadu Buhari unaolenga kukopa Dola bilioni 30 katika soko la kimataifa ili kuinua uchumi wa Nigeria.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (akivalia nguo nyeupe), pamoja na Makamu wa Rais, Yemi Osinbajo na mkurugenzi Mkuu wa shirika la Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde, Januari 5, 2016 Abuja.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari (akivalia nguo nyeupe), pamoja na Makamu wa Rais, Yemi Osinbajo na mkurugenzi Mkuu wa shirika la Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde, Januari 5, 2016 Abuja. PHILIP OJISUA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Buhari alisema wiki iliyopita kuwa anataka kutumia mkopo huu wa kuwekeza katika miundombinu na kilimo.

Kiwango cha mkopo ni kikubwa kuliko bajeti ya serikali ya Nigeria kwa mwaka 2016.

Wadadisi wanasema uamuzi wa Baraza la Seneti haupaswi kuchukuliwa kama kukataa, kwa sababu serikali inaweza kuwasilisha mpango mpya wa kukopa kwa maseneta.

Baraza la Seneti lilifutilia mbali mpango huo katika kikao kisiokua mjadala, Shirila la utangazaji la Reuters limesema.

"Hapana," wamesema kwa pamoja maseneta wengi, kwa mshangao mkubwa, wakati rais wa Baraza la Seneti, Bukola Saraki, aliomba kura mpya juu ya muswada huo.

"Mpango wa kukopa, ambao utatumika katika kipindi cha miaka mitatu unapaswa kusaidia Nigeria kuondokana na ukosefu wake miundombinu ulio dhahiri," ilisema taarifa ya serikali, ikimnukuu afisa wa idara inayohusika na urasibu wa madeni ya nje ya nchi .

Uchumi wa Nigeria ulianza kudororo tangu mwezi Agosti uliyopita kwa mara ya kwanza katika miaka zaidi ya 10 iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.