Pata taarifa kuu
AU-UCHAGUZI

Tume ya AU kukutana na wagombea 5

Uchaguzi wa wagombea watano ambao wanawania wadhfa wa uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AU unatarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka 2017, kumteuwa atakaye mrithi Nkosazana Dlamini-Zuma, raia wa Afrika Kusini, ambaye amekataa kuendeleza huduma yake kwa muhula wa pili.

Nkosazana Dlamini-Zuma, Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, katika mkutano na wandishi wa habari, mjni Addis-Ababa, Ethiopia..
Nkosazana Dlamini-Zuma, Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, katika mkutano na wandishi wa habari, mjni Addis-Ababa, Ethiopia.. REUTERS/Tiksa Negeri
Matangazo ya kibiashara

Kamati ya Umoja wa Afrika, imesema itafanya mkutano wake wa kwanza kwa wagombea watano ambao wanawania nafasi ya uenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika.

Wagombea watano wanaowania wadhifa wa Uenyekiti wa tume ya AU

1.Amina Mohamed, Waziri wa mambo ya Nje wa Kenya

2.Agapito Mba Mokuy, Waziri wa Mambo ya Nje wa Equatorial Guinea

3.Bathily Abdoulaye kutoka Senegal, ambaye kwa sasa ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

4.Pelonomi Venson-Moitoi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana

5.Moussa Faki Mahamat, Waziri wa mambo ya Nje wa Chad

"Tunaamini kwamba mjadala huu utatusaidia kubadilisha muungano na Afrika kwa ujumla, kama kawaida uchanguzi wa viongozi wa Umoja huu hufanyika kisiri huku wakiianya jamii yote ya Afrika nafasi ya kushiriki na kujumuika na kazi ya kamati hiyo, '' Kamati ya Umoja wa Afrika imesema katika taarifa yake.

Mualiko kutoka kwa kamati hiyo umesema , wagombea ambao wameonyesha nia yao katika kinyanganyiro hicho watashirikishwa katika mjadala utakao fanyika katika jumba la mikutano Desimba 9 katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini addis Ababa, nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.