Kundi la waasi la Avengers latangaza kusitisha vita Nigeria
Nchini Nigeria kundi la waasi la Avengers, lililoendesha mashambulizi kadhaa dhidi ya mitambo ya mafuta na gesi katika eneo la Niger Delta, limesema Jumatatu hii kuwa limesitisha mapigano dhidi ya serikali ya Nigeria.
Imechapishwa:
Katika taarifa iliyorushwa kwenye tovuti yake, kundi hili, hata hivyo, linasema linasubiri kauli kutoka kwa Rais Muhammadu Buhari ya kupanga upya na kuruhusu kila jimbo kujitawala.
"Wiki moja iliyopita, kundi la waasi la Avengers lilitangaza nia yake ya kuweka chini silaha na kuanza mazungumzo na serikali.
Mashambulizi yaliyokua yakiendeshwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kundi hili ambalo linadai ugawaji sawa wa utajiri limedhoofisha uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria, nchi ya kwanza barani Afrika kwa kuuza nje mafuta, ambapo kwa siku inauza mapipa 700,000.