Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO

Mazungumzo DRC: Upinzani wagawanyika

Mratibu wa mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Edem Kodjo, ametangaza kuanza kwa zoezi la maandalizi ya kamati ya mazungumzo Jumanne hii asubuhi katika mji wa Kinshasa.

Edem Kodjo wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini Kinshasa Juni 14, 2016.
Edem Kodjo wakati wa mkutano na vyombo vya habari mjini Kinshasa Juni 14, 2016. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Katika shughuli hizi, jopo la wanasiasa na wanaharakati wa asasi za kiraia watachagua hasa sehemu ambapo mikutano hii itafanyika, watu wanaopaswa kushiriki na lengo linalotafutwa.

Hata hivyo upinzani nchini DRC unaonekana kugawanyika kati ya wale ambao wanataka kushiriki mazungumzo bila masharti na wale wanaotoa masharti kabla ya kushiriki.

Chama cha MLC cha Jean-Pierre Bemba kimekataa katu katu wazo lolote la kufanya mazungumzo na serikali ilioko madarakani.

Muungano wa vyama vya upinzani unaoundwa na Etienne Tshisekedi na Moise Katumbi unakubaliana juu ya kanuni ya mazungumzo na umetoa masharti ya kushiriki mazungumzo hayo.

Muungano huo umeomba kuachiwa huru wale unaowachukulia kama wafungwa wa kisiasa.

rais Joseph Kabila amewaachia huru baadhi yao. Lakini muungano wa vyaa vya upinzani wa "Rassemblement" umesema idadi haitoshi.

Pia muungano huo unaomba Edem Kodjo, kuachia ngazi, kwani anaegemea upande wa serikali.

Edem Kodjo hivi karibuni aliungwa mkono na serikali ya Congo pamoja na Kanisa Katoliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.