Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA

Moise Katumbi atolea wito raia wa DRC kusalia nyumbani

Mwanasiasa wa upinzani, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Rais Joseph Kabila, Moise Katumbi Chapwe, amesema anaunga mkono tangazo la muungano wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa “Rassemblement” na kuwatolea raia wito wa kusalia nyumbani Jumanne Agosti 23.

Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi, wakati wa mahojiano Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi, wakati wa mahojiano Lubumbashi, Juni 2, 2015. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa vyama vya upinzani wa “Rassemblement” unadai kuungwaji mkono Katiba na uzingatiaji wa azimio 2277 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa;

Muungano huo pia unasema kuwa idadi ya wafungwa wa kisiasa ambao serikali imetangaza kuwachia huru haitoshi;

Vile vile muungano huo unalaani kuitishwa kwa Tume ya matayarisho ya mazungumzo na msuluhishi Edem Kodjo.

Muungano wa vyama vya upinzani wa “Rassembement umetolea wito raia kusalia nyumbani kwa siku ya Jumanne tarehe 23 Agosti.

Moise Katumbi, katika tangazo alilolitoa Jumatatu jioni anasema ni muhimu kwa kupinga ujanja wa serikali ambao unaonyesha wazi kuwa ni uonga wa kisiasa, wakati ambapo imeendelea na mpango wake wa kuwakandamiza kiholela wafuasi wa vyama vya upinzani na kushawishi vyombo vya sheria.

Moise Katumbi Chapwe anasema kuachiliwa huru kwa watu wanne wasio kuwa na hatia ni ujanja wa serikali wakati ambapo bado kuna mamia ya wanasiasa wanaendelea kusalia katika magereza mbalimbali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Masharti ya kushiriki katika mazungumzo yaliyotolewa na muungano wa vyama vya upinzani wa "Rassemblement" wakati wa mkutano wa mjini Genval bado ni vigumu kutekelezwa. Kuitishwa kwa Tume ya matayarisho ya mazungumzo na Msuluhishi Edem Kodjo ni jambo lisilokubalika na ni uchochezi dhidi ya raia wa Congo, amesema Moise Katumbi.

Kwa hiyo, naitikia wito wa muungano wa vyama vya upinzani wa "Rassemblement" kwa kusalia nyumbani kwa siku ya Jumanne, Agosti 23, 2016 nchini kote DRC. Natoa witokwa raia wa Congo wanataka kudumisha demokrasia kusema HAPANA kwa kusogeza mbele kalenda ya uchaguzi, ameongeza Bw Katumbi Chapwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.