Pata taarifa kuu
DRC-HRW

Mwakilishi wa HRW nchini DRC alazimishwa kuondoka

Ida Sawyer aliondoka Jumanne usiku, Agosti 9, baada ya miaka minane nchini humo, ambapo kuondoka kwake kumetokana na Serikali kumnyima Visa ya kuendelea kuishi na kufanya kazi nchini DRC.

Nembo ya shirika la kimataifa la haki zabinadamu la Human wrights watch
Nembo ya shirika la kimataifa la haki zabinadamu la Human wrights watch hrw.org
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa HRW hakuwa na njia nyingine na kulazimika kuondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Muda wa viza yake ilikua umekwisha. Viza yake nyingine iliku ilisahihishwa mwezi Mei na muda wake ungelimalizika hadi mwaka 2019, lakini ilifutwa mwezi uliopita.

Ida Sawyer aliomba apewe viza nyingine, lakini alikataliwa. Kwa upande wa shirika la kimataifa la haki la Human Rights Watch, limesea uamuzi huo ni njia ya kukandamiza sauti ya wale wote ambao wanakemea ukandamizaji na mauaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa kipindi chote cha miaka minane, Ida Sawyer alisaidia kuandika ripoti nyingi, ikiwa ni pamoja na kulaani shinikizo kwa upinzani na vyama vya kiraia. Hali ya ya wasiwasi inaendelea kushuhudiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kukaribia tarehe iliyopangwa kwa uchaguzi wa urais. Kulingana na Katiba uchaguzi unapaswa kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka.

Adhabu ya kisiasa kwa HRW

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch linasema halina mashaka: Ida Sawyer ameadhibiwa kwa sababu alikua akilaani vitendo vingi viovu dhidi ya raia. Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo katika ukanda wa Afrika, Van Woudenberg, ameshutumu uamuzi huo na amesema kusikitishwa kwamba serikali ya Dr Congo haikutoa maelezo.

Kwa upande wake, Msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende, amebainisha kuwa mamlaka ya uhamiaji haina haja ya kueleza uamuzi wake. "Mamlaka ya uhamiaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wana uwezo wa kukubali au kukataa maombi au kufuta viza iliyotolewa kwa raia kigeni, bila ya sisi kutakiwa kutoa maelezo," Lambert Mende ameiambia RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.