Pata taarifa kuu
DRC-MALUKU-MAUAJI-KUFUKULIWA

Kaburi la pamoja la Maluku DRC: familia zadai kufukuliwa kwa maiti

Mpaka sasa mwanga haujatolewa kuhusu miili 421 ya watu iliyozikwa Machi 19 kwenye kaburi la pamoja la Maluku, kilomita 80 na mji wa Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Makaburi ya Maluku, ambapo miili ya watu 421 ilizikwa Machi 19 mwaka 2015 usiku.
Makaburi ya Maluku, ambapo miili ya watu 421 ilizikwa Machi 19 mwaka 2015 usiku. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Miezi miwili tangu kesi hiyo kufunguliwa, shirika la kimataifa la haki za binadamu Human Right Watch limeomba likisisitiza wito uliyotolewa na familia 34, ambazo zimeomba viongozi kufanya kiliyo chini ya uwezo wao ili kaburi hilo lifukuliwe kwa minajili ya kuchunguza kama kweli watu hao waliouawa au kutoweka mwezi Novemba na Januari ni ndugu zao ambao walizikwa sehemu hiyo.

“ Sisi [...] tunaomba kuwepo na uchunguzi uliyohuru na wazi kuhusu miili ya watu iliyozikwa kwenye kaburi la Maluku, bila hata hivyo kuweko na sababu za kisiasa. Wachunguzi na wataalam wa kimataifa na wale wanaojitegemea wanatakiwa kushirikishwa katika uchunguzi huo, huku vipimo vya vinasaba vikipewa kipao mbele”. Hayo ni miongoni mwa yaliyomo kwenye barua ya mashtaka familia 34 ziliyomuandikia Ijumaa Juni 5 mwendesha mashtaka wa taifa.

Familia 12 miongoni mwa familia hizo ziliwapoteza ndugu zao baada ya maandamano ya mwezi Januari, huku familia 26 pia zikiwakosa ndugu zao baada ya operesheni dhidi ya uhalifu iliyojulikana kwa jina la Likofi iliyoendeshwa mwishoni mwa mwaka 2013 katika mji wa Kinshasa.

Mpaka sasa hakuna familia hata miongoni mwa familia hizo iliyopewa maiti ya ndugu zao. Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch limeamua miili hiyo kaburi hilo lifukuliwe.

“ Mpaka sasa mwanga haujatolewa kuhusu miili ya watu iliyozikwa kwenye kaburi la pamoja la Maluku. Kwa hiyo tunafikiri kuwa ni muhimu kwa viongozi wa Congo kufanya haraka ili kujua ni miili ya watu gani iliyozikwa kwenye kaburi hilo la pamoja”, amesema Ida Sawyer, mtafiti wa Human Right Watch.

Itafahamika kwamba Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, na hivi karibuni naibu waziri wa haki za binadamu wa Marekani, Tom Malinowski, pia wameomba kaburi la Maluku lifukuliwe, bila mafanikio mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.