Pata taarifa kuu
LIBYA-SERIKALI YA UMOJA

Libya: Bunge kupiga kura ya kuunga mkono serikali ya kitaifa

Jumatatu hii Aprili 18, Bunge nchini Libya linapiga kura ya kuonyesha imani na kuiunga mkono serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa.

Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco.
Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya Bunge la Libya inakuja huku Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond akifanya ziara ya kushtukiza nchini humo.

Hammond anakuwa mwanadiplomasia mwingine wa juu kuzuru nchi hiyo baada ya Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka Italia, Ufaransa na Ujerumani kuzuru Tripoli kuiunga mkono serikali hiyo.

Ziara hii inaashiria kuwa Jumuiya ya Kimataifa inaiunga mkono serikali hiyo ya umoja wa kitaifa inayolenga kumaliza machafuko nchini humo na kufanikiwa vita dhidi ya makundi ya wanajihadi.

Waziri Mkuu Mtarajiwa Fayez Sarraj, katika siku za hivi karibuni amekuwa akiendelea kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa makundi mbalimbali nchini humo.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo huu Martin Kobler akiwa mjini Tobruk linaloketi bunge hilo amesema ameridhishwa na idadi kubwa ya wabunge wanaonekana wakiwa tayari kushiriki katika zoezi la upigaji kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.