Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

BCL na NOC vyaunganisha serikali ya umoja Libya

Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya imeimarisha nguvu zake Jumapili hii na kupata uungwaji mkono wa taasisi mbili muhimu, ikiwa ni pamoja na Benki Kuu, ambayo ni taasisi ya Fedha na Kampuni ya kitaifa ya mafuta (NOC) inayosimamia rasilimali kuu ya nchi hiyo.

Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco.
Waziri Mkuu mteule wa Libya, Fayez el-Sarraj (kushoto), Februari 15, 2016 katika mji wa Skhirat, Morocco. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Uungwaji huu mokono muhimu katika ngazi ya fedha na uchumi unaipa kisogo serikali ya Tripoli isiotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, lakini pia ile inayoendesha shughuli zake mashariki mwa nchi.

Serikali hizi hasimu ambazo mpaka sasa zimekua zikiongoza Libya zimekataa kuachia madaraka kwa serikali ya umoja ambayo iliundwa Ijumaa kwa msaada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ambapo Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj ameanza kuhudumu kwenye wadhifa huo mjini Tripoli tangu Jumatano Machi 30.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili hii, Benki Kuu ya Libya (BCL) "inakaribisha" kuwasili kwa serikali ya umoja "na maazimio ya Baraza la Usalama" ya Umoja wa Mataifa.

"Ni wajibu wetu sote kufanya kazi kwa bidii kwa umoja wa nchi yetu na kuipa matumaini Libya (...), kwa kusaidia uchumi na kuongeza uzalishaji na mauzo ya mafuta nje ya nchi( ...), " BCL imeongeza.

Kabla ya Benki Kuu, Kampuni ya kitaifa ya mafuta pia iliunga mkono serikali ya umoja.

"Tunafanya kazi na Waziri Mkuu (Fayez) al-Sarraj pamoja na Ofisi ya rais kwa kuweka kando tofauti zetu," Mustafa Sanalla, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kitaifa ya mafutakatika, amesema atika taarifa yake.

"Kwa sasa tuna mfumo wa kisheria wa kimataifa kwa kufanya kazi," Mustafa Sanalla ameongeza, akimaanisha uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa kwa serikali ya Sarraj.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.