Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MALI-USHIRIKIANO

Ujerumani yajikubalisha kuisaidia Mali

Tangazo la dhamira ya ziada ya Ujerumani lilikua lilipangwa kabla ya mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris. Lakini mashambulizi haya yaliisukuma Berlin kwenda mbali zaidi ili kusaidia na kuipongeza Paris katika mapambano yake dhidi ya ugaidi.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani katika kambi ya kikosi cha wanaanga ya Incirlik (Uturuki), Januari 21, 2016.
Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani katika kambi ya kikosi cha wanaanga ya Incirlik (Uturuki), Januari 21, 2016. © REUTERS/Tobias Schwarz/Pool
Matangazo ya kibiashara

Baada ya uamuzi wa serikali ya Ujerumani mapema mwezi huu, bunge limepiga kura Alhamisi hii, Januari 28 kwa neema ya muhula mpya unaoongeza ushiriki wa Bundeswehr katika kikosi cha wanajeshi wa umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA).

Vyama vyote ispokua kile cha mrengo wa kushoto cha Die Linke, vimepitisha muhula huo mpya wa mwaka mmoja. Muhula huo mpya umepitishwa kwa kura 502 kwa jumla ya wapiga kura 574. Ushiriki wa Ujerumani katika kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa mataifa nchini Mali (MiNUSMA) umeongezeka kutoka askari 150 hadi 650. Askari kadhaa ndio wameshatumwa pekee mpaka sasa. Karibu askari 400 wako mbioni kutumwa kaskazini mwa Mali ifikapo mwezi Juni.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Ursula von der Leyen, amezungumza katika mahojiano kwamba poeresheni hii ya kudumu imepasishwa kutokana na hatari ambayo inaweza kutokea wakati wowote. Msemaji wa kundi la wabunge kutoka chama cha Social Democratic, Niels Annen, ametetea operesheni jhii Alhamisi hii katika Bunge la Ujerumani (Bundestag).

"Ongezeko kubwa la ushiriki wa Bundeswehr katika Minusma nchini Mali ni ishara kubwa. Hatuwezi kuendelea tonatofautiana kwa kile kinachotokea katika bara la Afrika, amabao jirani zetu. Kwa sababutumejikuta kuwa usalama wetu kwa pande zote za Bahari ni uhusiano wa karibu. Ni kweli, ni utaratibu hatari. Lakini tukilinganisha na Afghanistan kwa jinsi tulivyosikia na kusoma kwenye vyombo vya habari vya Ujerumani kuna mambo ambayo wamezidisha", amesema Niels Annen.

Mbali na ushiriki katika kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa (MINUSMA), Ujerumani imejikubalisha kutuma askari 200 kwa ujumbe wa Ulaya kuhusu mafunzo ya jesi la Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.