Pata taarifa kuu
BURUNDI-UNSC-USALAMA

Pierre Nkurunziza habadili msimamo wake mbele ya UNSC

Ziara ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nchini Burundi imemalizika Ijumaa hii kwa mkutano na Rais Pierre Nkuruzniza mjini Gitega, katikati mwa nchi hiyo. Baada ya ziara hio iliyodumu saa 42, kila upande umeendelea kushikilia msimamo wake.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa mjini Bujumbura, Januari 22, 2016.
Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, pamoja na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa mjini Bujumbura, Januari 22, 2016. © AFP / ONESPHORE NIBIGIRA
Matangazo ya kibiashara

Pierre Nkurunziza amefutilia mbali kata kata uwezekano wa kutumwa kwa kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika kwa kuwalindia usalama raia. “Msaada ambao Burundi inahitaji sio wa kijeshi”, amesema Rais Pierre Nkurunziza, kama alivyobaini msemaji wake, Karerwa Ndenzako kwenye Twitter.

Vile vile hakuna haja ya mazungumzo na watu waliohusika katika jaribio la mapinduzi au upinzani ulio uhamishoni. “ Njia pekee ya amani na demokrasia ni kuwakamata na kuwahukumu wale waliohusika na kuchochea vurugu popote pale walipo”, amesema Rais wa Burundi

Kuhusu uchunguzi uliopendekezwa na Umoja wa Mataifa kufuatia ripoti kuhusu ubakaji, mateso, mauaji na uwepo wa makaburi ya halaiki, Pierre Nkurunziza hakuahidi chochote. “Burundi iko huru, na itategemea iwapo serikali itatoa idhni ya kufanyika kwa uchunguzi huo”, amejibu. Lakini kwa upande wa Rais Pierre Nkurunziza mauaji ya kimbari “ni kisingizio”.

Mchana kutwa, viongozi wa Burundi wametaka kuonyesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa hali ya nchi ni nzuri. Wafusai wa chama tawala cha CNDD-FDD walihamasishwa Alhamisi wiki hii kwenda kuupokea ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura. Lakini cha kushangaza ni kwamba kwenye mabango waliokua wakibebelea kulikua kuliandikwa kwa lugha ya Kingereza “Burundi ni nchi huru”, “achane kuigilia masuala ya ndani ya Burundi” au pia: “hakutokuepo na mauaji ya kimbari nchini Burundi”.

“Karibuni sana Burundi, nchi tofauti na vile mlivyokua mkisikia wakizungumza”, ameendelea kusema Rais Nkurunziza kama maeneo ya utangulizi wa mkutano na wawakilishi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baada ya usiku wa machafuko yaliogharimu maisha ya watu watatu na kuwajeruhi watu 13 mjini Bujumbura, Barazala la Usalama la Umoja wa Mataifa walikutana na viongozi husika tofauti, ikiwa ni pamoja na Makamu wa kwanza wa rais Gaston Sindimwo, ambaye amewahakikishia Wawakilishi hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba serikali pia ina wasiwasi na hali inayojiri Burundi, na anapania kuanzisha ushirikiano pamoja na Umoja wa Matiafa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana baadaye na wawakilishi wa vyama vya kiraia na upinzani uliosalia mjini Bujumbura. Upinzani ambao una matumaini kwa ziara ya ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa nchini humo.

Mmoja wa wajumbe wa upinzani amaesema kuwa ana imani na ziara hiyo ya ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa mambo matatu yataulu: mazungumzo yatakayozishirikisha pande zote husika katika mgogoro wa Burundi, ikiwa ni pamoja na upinzani ulio ukimbizini, uchunguzi kuhusu kuwepo kwa makaburi ya halaiki na kutumwa kwa kikosi cha askari wa Umoja wa Afrika kuwalindi usalama raia.

Hata hivyo inaonekana kuwa matumaini hayo yameklua kama ndoto, kwani Rais Pierre Nkurunziza amekataa katu katu mambo hayo matatu katika mkutanop na ujumbe wa Baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa matumaini yako upande wa ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utakaowasilisha Jumamosi hii kwa Umoja wa Afrika. Wajumbe wake waliondoka mjini Bujumbura Ijumaa hii na wanakutana kwa sasa na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.