Pata taarifa kuu
MALI-MASHAMBULIZI-USALAMA

Mali: Massina yakiri kutekeleza mashambulizi dhidi ya hoteli Radisson

Katika taarifa iliotumwa kwenye ofisi ya RFI / AFP jijini Bamako, kundi la waasi la Massina limetibitish kwamba wapiganaji wake waliendesha shambulizi la kigaidi lililogharimu maisha ya watu 21 Ijumaa wiki iliyopita katika hoteli Radisson katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Rais wa Senegal Macky Sall (katikati) na mwenzake wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kulia) na mkurugeni wa hoteli Radisson (kushito), Novemba 22, 2015 jijini Bamako.
Rais wa Senegal Macky Sall (katikati) na mwenzake wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (kulia) na mkurugeni wa hoteli Radisson (kushito), Novemba 22, 2015 jijini Bamako. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa kundi hilo la waasi, amesema kitendo hiki "ni ulipizaji kisasi kwa mashambulizi ya kikosi cha Ufaransa kiliotumwa Mali Barkane kwa ushirikiano na jeshi la Mali, yanayoendelea kuwalenga wafuasi na maafisa wa makundi ya FLM na Ansar Dine".

Jumamosi, kundi la waasi linalongozwa na Mokhtar Belmokhtar, al-Mourabitoune lilikiri kuendesha mashambulizi katika hoteli Radisson.
Baada ya mashambulizi yaliogharimu hayo Ijumaa Novemba 20, Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta aliitisha kikako cha dharura cha Baraza la Mawaziri.

Rais wa Mali alitangaza hali ya hatari kwa muda wa siku kumi na siku tatu za maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya watu waliouawa katika mashambulizi hayo.

Hatua hizi zilichukuliwa katika kikako cha dharura cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa hadi Ijumaa jioni na Rais Ibrahim Boubacar Keïta, ambaye alirejea nchini mwake alasiri akitokea katika mkutano wa nchi za Sahel jijini Ndjamena, nchini Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.