Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Serikali ya Mali yaghadhabishwa na hatua ya UN

Serikali ya Mali imeelezea wasiwasi wake kufuatia hatua zilizochukuliwa na vikosi vya Umoja wa mataifa vya kulinda amani nchini Mali (Minusma) kwa kutenga eneo la kilomita mraba 20 kukabiliana na hali ya usalama katika mkoa Kidal.

Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji waKidal, 22 Julai mwaka 2015.
Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji waKidal, 22 Julai mwaka 2015. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vinatazamia pia kulinda wakaazi wa eneo hilo ambapo makundi ya waasi wa Azawad na wengine yanasababisha ukosefu wa usalama licha ya makubaliano ya amani yaliyosainiwa miezi miwili iliyopita.

Hatua hiyo inaighadhabisha serikali ya Bamako kwa kuchukuliwa bila ya kushauriana baina ya serikali ya nchi na vikosi hivyo.

Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema umewatuma wanajeshi wake katika mji wa Kidal, Kaskazini mwa Mali. Uamzi huu umechukuliwa ili kuzuia kuenea kwa mapigano ambayo yamesababisha vifo vingi Jumatatu Agosti 17 kilomita 120 na mji huo, mapigano ambayo yalizuka kati ya makundi hasimu.

Kama ilivyotarajiwa, askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walianza kupelekwa kwenye umbali wa kilomita 20 na mji wa Kidali ili waweze kuulinda mji huo na mapigano yanayoendelea katika maeneo jirani . " Mambo yote yanakwenda sawa, hakuna matatizo ", amesema afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa alipowasiliana na RFI kwa njia ya simu.

Masaa ishirini na nne baada ya mji wa Anefis kudhibitwa na wapiganaji wa makundi yanayounga mkono serikali, hali ya utulivu imeanza kurejea, kwa mujibu wa mashahidi wawili waliohojiwa tofauti. Kwa sasa bendera ya taifa inaelea katika mji wa Anefis, mji unaopatikana kwenye umbali wa zaidi ya kilomita mia moja kusini mwa mji wa Kidal.ya mji ni yaliyo bendera ya taifa.

Mbali kidogo, kaskazini mwa mji wa Kidal, katika mji wa el-Gerer, eneo lingine ambapo makundi hasimu yamekua yakiendelea na mapigano kwa muda wa siku tatu, hali ya utulivu pia imerejea, lakini hali ya taharuki imetanda, kwa mujibu wa chanzo cha kigeni, ambacho kinahofu ya kutokea kwa mapigano mapya.

Mjini Bamako, baadhi ya maafisa wa serikali wanasema kughadhabishwa na ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji mapigano unaofanywa na washirika wao ambao wamekua wakiendesha vita dhidi ya waasi wa Azawad , viongozi hao wamekumbusha kwamba hivi karibuni rais Ibrahim Boubacar Keita amekuatana kwa mazungumzo kwa muda mrefu na wawakilishi wa waasi wa Azawad na kuwaeleza nia yake ya kuheshimu ahadi zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.