Pata taarifa kuu
NIGER-UCHAGUZI-SIASA

Niger: chama kikuu cha upinzani chamteua mgombea wake

Chama kikuu cha upinzani nchini Niger, kimemteua Hama Amadou, kiongozi anayeishi uhamishoni, na ambaye aliwahi kuwa spika wa bunge, kushindana na rais Mahamadou Issoufou kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Hama Amadou ameteuliwa kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais ujao Niger kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani cha MDN..
Hama Amadou ameteuliwa kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais ujao Niger kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani cha MDN.. AFP PHOTO STEPHANE DE SAKUTIN
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili la uteuzi huu lililotolewa na chama cha MDN, baada ya kufanyika kwa mkutano mkubwa wa chama siku ya jumapili mwishoni mwa juma lililopita.

Wajumbe wa kiongozi huyo na wafuasi wa chama hicho wamesema kuwa Amadou ni mzoefu wa siasa za Niger, wala hakuna pingazi zozote.

“ Sote tumekubaliana na tumeridhika kumteua Amadou kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama cha MDN ”, amesema mmoja kati ya wafuasi wa chama hicho.

Amadou yuko nchini Ufaransa ambako ameomba hifadhi baada ya kukimbia nchi yake mwaka 2014 kufuatia bunge la nchi hiyo kumuondolea kinga kutokana na kashfa ya kuuza watoto wachanga, tuhuma ambazo wafuasi wake wanasema zimechochewa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.