Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-USALAMA

Niger: Boko Haram yatekeleza mashambulizi

Pamoja na kushindwa katika maeneo ya yaliyopembezoni mwa ziwa Chad, Boko Haram imeanza kutumia mbinu nyingine katika vita inavyoendesha.

Vijiji viwili viliyoshambuliwa vinapatikana katika jimbo la Diffa, karibu na mpaka na Nigeria.
Vijiji viwili viliyoshambuliwa vinapatikana katika jimbo la Diffa, karibu na mpaka na Nigeria. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa Boko Haram wameanza kuendesha mashambulizi katika maeneo yasiyo lindwa na jeshi aidha polisi. Kundi hili limeendesha mashambulizi katika vijiji viwili nchini Niger usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi wiki hii, na kusababisha vifo vya watu 38.

Vijiji viliyoshambuliwa na Boko Haram ni pamoja na Lamana na Ngoumao. Vijiji hivyo vilikua havilindwi na vikosi vya usalama na jeshi, kwani ngome za jeshi za Damasak na Malan Fatori ziko mbali zaidi na vijiji hivyo viliyoshambuliwa.

Baada ya mauaji hayo wapiganaji wa Boko Haram walitoweka msituni biala hata hivyo kukabiliana na vikosi ya usalama. Watu 38 wameuawa na wengine wengi wamejeruhiwa, huku vijiji vya Lamana et Ngoumao vikiteketezwa kwa moto.

Ikiwa ni mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhan, mashambulizi haya yamewatia hofu raia wanaoishi karibu na mto Komadugu Yobe. Mkuu wa jimbo la hilo na ujumbe wake walienda kuwaunga mkono raia hao. Wanakijiji wameomba usalam wao uimarishwe vya kutosha, au ikiwezekana wahamishiwe katika maeneo mengine.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, wapiganaji wa Boko Haram, ambao walishambuliwa vijiji hivyo ni vijana wazaliwa wa eneo hilo, na wanajua vizuri maeneo yasiyolindwa na vikosi vya vya usalama.

Wadadisi wamebaini kwamba kama jeshi la nchi jirani ya Nigeria litakuwa bado halijatoa ulinzi wa kutosha kwenye mipaka yake, mashambulizi ya Boko Haram yataendelea kushuhudiwa katika nchi ya Niger.

Kikosi cha kimataifa cha kikanda chenye wanajeshi 8,000 kinasubiriwa ili kukabiliana na Boko Haram katika nchi jirani na Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.