Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-MAPIGANO-USALAMA

Serikali ya Niger yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu

Nchi ya Niger imeanza Jumatano wiki hii kipindi cha siku tatu cha maombolezo ya kitaifa ambapo bendera ya taifa hilo itapepea nusu mlingoti kufwatia vifo vya askari wasiopungua 40 waliouawa katika makabiliano ya hivi karibuni dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad.

Mahamadou Issoufou, rais wa Niger.
Mahamadou Issoufou, rais wa Niger. France 24
Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Ufaransa imekuwa bega kwa bega na nchi hiyo katika maombolezo hayo kupitia kwa Katibu mkuu wa Wizara ya maendeleo na Francophonie Bi. Annick Girardin aliyemaliza ziara yake hapo jan Jumanne katika ukanda wa Afrika Magharibi na kuahidi ushirikiano wa nchi yake katika vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

Wanajeshi hao walikua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga, katika ziwa Chad. Kundi la kiislamu la Boko Haram ililiendesha shambulio mapema Jumamosi asubuhi dhidi ya wanajeshi 120 waliokua wakipiga kambi katika kisiwa cha Karamga, kwenye mwambao wa ziwa Chad. Wanajeshi wa Niger waliamua kutimka baada ya kuzidiwa nguvu. Inaarifiwa kuwa shambulio hilo liliendesha na zaidi ya wapiganaji 2000 wa Boko Haram, ambao walikua na zana nzito za kijeshi. Kwa sasa kisiwa hicho cha Karamga kinashikiliwa na Boko Haram.

Kwa mujibu wa mashahidi katika mji wa Diffa, mji mkuu wa jimbo la kusini mashariki mwa Nigeria, mapigano hayo yaligharimu maisha ya wanajeshi 48 wa Niger na wengine 36 hawajulikani walipo. Itakua ni pigo kubwa kwa serikali ya Niger iwapo taarifa hii itathibitishwa. Awali wizara ya ulinzi ilithibitisha kutokea kwa mapigano kati ya jeshi na wanamgambo wa Boko Haram, lakini hakuna idadi ya hasara iliyotolewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.