Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-MAPIGANO-USALAMA

Niger: Diffa, raia waishi kwa hofu ya kuuawa na Boko Haram

Sehemu ya kwanza ya mfululizo wa taarifa zetu juu ya hali inayojiri kusini mwa Niger. Mji wa Diffa umeendelea kuwa uwanja wa mapambano ya hapa na pale tangu kupelekwa kikosi kikubwa cha wanajeshi kutoka Niger mwezi Mei.

Yacouba Soumana Gaoh, mkuu wa jimbo la Diffa, Niger.
Yacouba Soumana Gaoh, mkuu wa jimbo la Diffa, Niger. PAM / Tim Dirven
Matangazo ya kibiashara

Lakini mji huu bado umeendelea kulengwa na mashambulizi ya Boko Haram. Kwa kushambulia gereza, wapiganaji wa kundi la Boko Haram pengine wamekua wakijaribu kuwatorosha baadhi ya wenzao wanaozuiliwa katika geraza la mji wa Diffa. Hii pia ni sababu mojawapo ya watu wanao shukiwa kuwa na uhusiano na kundi hili la Boko Haram au kuwa washirika wa kundi hili hupelekwa moja kwa moja katika mji wa Niamey. Hata hivyo, mji wa Diffa unakabiliwa na hali ya sintofahamu na huenda hali hii ikawaathiri wakaazi wa mji huo.

Katika mji wa Diffa na maeneo jirani, siku tatu haziwezi kupita bila kutokea kwa mashambulizi au uvamizi ambao Boko Haram hujaribu kutekeleza. Licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Niger katika mji huu, uvumi umeendelea kusambaa. Boko Haram inataka kuudhibiti mji huu au kutenda shambulio baya litakalosababisha maafa makubwa kabla ya mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan.

Hofu imetanda katika mji huu kuanzia kwa viongozi hadi raia. Hali hii imepelekea viongozi kuchukua mkakati wa kulihusisha kundi la watu kwamba wanashirikiana na kundi hili.

" Tunawakamata watu kwa misingi ya ushahidi au taarifa mbalimbali ", amesema Yacouba Soumana Gaoh, mkuu wa mkoa wa Diffa.

" Mtu akishukiwa tu, tunaambiwa. Mtu huyu anakabiliwa na tuhuma fulani. Kwa Muislamu yeyote, wakati unapoinua Koran, huweza kuficha chochote. Nina wazazi ambao walikuja hapa ofisini mwangu na watoto wao waliowazaa, na kusema kuwa alikuwa kwenye uwanja wa vita au mwanangu amejificha eneo fulani. Hivyo ndivy tunavyokamata watu ", ameedelea kusema Yacouba Soumana Gaoh.
Vijana wapotea kutoka Bagara.

Kwenye umbali wa kilomita kadhaa kutoka Diffa, kati ya mji na mto Komadougou, ambao ni mpaka na nchi ya Nigeria, kuna kijiji kidogo cha Bagara ambapo vijana wa kijiji hiki wameondoka na kumejiunga na kundi la Boko Haram na wengine wanazuiliwa jela katika mji wa Niamey.

Wazazi wengi wamekua wakibaini kwamba wanao wamekua wakizuiliwa Bagara na kupelekwa katika mji wa Niamey, huku wazazi wengine wakibaini kwamba wanao wamekamatwa baada ya kusotewa kidole na baadhi ya watu kwa wanajeshi kwamba walikua wapiganaji wa kundi la Boko Haram. " Kwa sasa vijana hao wanazuiliwa katika jela la mji wa Niamey ", wamesema baadhi ya wazazi waliozungumza na RFI.

Vijana wanaokamatwa kwa tuhuma mbalimbali, ikiwa ni kushiikiana na Boko Haram au kushukiwa kuwa na uhusiano na kundi hili, hupelekwa katika mji wa Niamey ambapo wanahojiwa kwa siku kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.