Pata taarifa kuu
ALGERIA-USALAMA

Algeria: Bouteflika amstaafisha mkuu wa ujasusi

Nchini Algeria, mkuu wa Idara ya ujasusi, jenerali Médiène, anayejulikana kwa jina la "jenerali Toufik", amestaafishwa na Rais Abdelaziz Bouteflika. Jenerali Toufik amekuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 25. Uamzi huo wa kustaafishwa kwa afisa huyo unakuja wakati Idara hiyo ya ujasusi imeboreshwa kwa mwaka mzima sasa.

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika mwezi Disemba, 2011.
Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika mwezi Disemba, 2011. FAROUK BATICHE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ni mtu asiyefahamika, ambaye raia wengi wa Algeria hawamtambui, ambapo picha yake ya mwisho ilionekana katika miaka ya 1990, lakini anajulikana kuwa ni mmoja wa viongozi mashuhuri wenye ushawishi mkubwa nchini humo.

Jenerali Mohamed Médiène, mwenye umri wa miaka 76, amestaafishwa baada ya kuongoza Idara ya ujasusi nchini Algeria kwa kipindi cha miaka 25. Jenerali Athmane Tartag, amemrudilia nafasi yake. Jenerali Athmane Tartag ana sifa za mtu mwenye jeuri. Anajulikana kuwa aliongoza katika miaka ya 1990 kituo cha uchunguzi wa kijeshi, kituo ambacho wanamgambo wa Kiislam wanadaiwa kufanyiwa mateso kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Jenerali Tartag alikuwa ameshastaafu. Hii inaonyeshwa na baadhi ya waangalizi kwamba huu sio mwisho wa jenerali Toufik.

Hata hivyo, kwa miezi kadhaa, Idara ya ujasusi ya Algeria imefanyiwa mabadiliko, ambapo vitengo kadhaa viliwekwa chini ya udhibiti wa Ofisi ya rais wa Jamhuri. Na kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Algeria, mabadiliko hayo yameidhoofisha Idara ya ujasusi, kwa faida ya Abdelaziz Bouteflika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.